Ujerumani yaisambaratisha Uingereza
29 Juni 2010Matangazo
Uingereza ilikataliwa bao lake la kusawazisha, la mkwaju wa Frank Lampard, lakini hata hivyo ilishindwa kabisa kuzuia kasi ya wachezaji wa Ujerumani.
Mabao ya Ujerumani yaliwekwa wavuni na Mirosla Klose, Lukas Podoski na Thomas Muller aliyepachika mawili.
Katika mechi hiyo iliyokuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa kote duniani, mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller alichaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mechi.
Ujerumani sasa itapambana na mshindi kati ya Argentina na Mexico.
Mwandishi:Aboubakary Liongo