Ujerumani yaiomba Syria kutumia ushawishi wake ili Lebanon imchague rais
18 Januari 2008Matangazo
BERLIN:
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani-Frank-Walter Steinmeier-ameihimiza Syria kutumia ushawishi wake kuwezesha kuchaguliwa kwa rais nchini Lebanon na pia kuwashawishi wapiganaji wa kundi la Kipalestina la Hamas kukomesha kuvurumisha maroketi nchini Israel.
Bw Sterinmeier amelaumiwa na Marekani na Lebanon kwa kumkaribisha mjini Berlin, cheo somo wake wa Syria, jana alhamisi.
Waziri ametetea mkutano wake akisema Syria inauwezo, aidha wa kusiaidia au kuvuruga , mchakato mzima wa amani ya mashariki ya kati.Marekani inataka Syria itengwe kutokana na jinsi inavyovuruga Lebanon na pia uungaji wake mkono makundi yenye siasa kali ambayo yanahusika na visa vya kuivuruga Israel.