Ujerumani yaingia robo fainali UEFA 2012
18 Juni 2012Matangazo
Ujerumani imetinga hatua hiyo baada ya kuiadhibu Denmark bao 2-1 kwenye mchezo wa jana, huku Ureno nayo ikiitoa nje ya mashindano Uholanzi kwa kipigo cha namna hiyo cha bao 2-1. Ujerumani ndiyo kinara wa kundi B kwa pointi 9, ikifuatiwa na Uholanzi yenye pointi 6. Kwa matokeo hayo, sasa Ujerumani itakwaana na Ugiriki kwenye mchezo wa robo fainali. Ugiriki ndiyo iliyoifanya Urusi ifunge virago vyake Jumamosi iliyopita baada ya kuichapa bao 1-0.
Mwandishi: Stumai George
Mhariri: Oummilkheir Hamidou