Ujerumani yailaza Uingereza bao nne kwa moja.
28 Juni 2010Matangazo
Mashindano ya kombe la dunia ya soka yanaendelea leo nchini Afrika kusini, baada ya timu mbili za Ujerumani na Argentina jana kufanikiwa kuingia robo fainali za mashindano hayo.
Ujerumani ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kuibamiza Uingereza mabao manne kwa moja, ambapo magoli yake yalifungwa na Miroslav Klose na Lukas Podolski katika kipindi cha kwanza na mengine mawili yalifungwa na Thomas Mueller katika kipindi cha pili.
Goli la Uingereza la kufutia machozi lilifungwa na Matthew Upson.
Na katika mchezo mwingine uliochezwa hapo jana, Argentina nayo iliweza kusonga mbele kwa kuifunga Mexico, mabao matatu kwa moja.
Argentina itapambana na Ujerumani katika robo fainali, Jumamosi ijayo.