Ujerumani yaridhia kuongezwa muda kwa oparesheni ya ulinzi
22 Machi 2024Bunge la Ujerumani Bundestag jana lilipiga kura na kuunga mkono kuongezwa muda wa kuhudumu kwa wanajeshi hao.
Oparesheni hiyo ya kimataifa ya ulinzi katika bahari ya Mediterania inalenga kukabiliana na ugaidi na biashara ya magendo ya silaha.
Soma pia: Scholz asisitiza msimamo wake wa kutoipa Ukraine makombora ya Taurus
Bunge hilo la Ujerumani pia lilijadili juu ya kuongeza muda wa wanajeshi wa Ujerumani katika ushirikiano wao na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.
Hadi askari 50 wa Ujerumani wanaweza kushiriki katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo ili kuhakikisha usalama wa raia.
Licha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kukamilika rasmi kufuatia makubaliano ya amani ya mwaka 2008, makundi kadhaa yenye silaha bado yanapigana kutafuta uhalali wa kujumuishwa kwenye serikali.