1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaelekea Ufaransa katika Euro 2016

Admin.WagnerD6 Juni 2016

Mabingwa wa dunia Ujerumani wameondoka kuelekea Ufaransa katika kambi yao ya michuano ya Euro 2016 wakiwa matumaini makubwa baada ya kuishinda Hungary 2-0 mjini Gelsenkirchen mwishoni mwa wiki

https://p.dw.com/p/1J1Om
Schweiz Training der Deutschen Fußballnationalmannschaft in Ascona
Picha: Reuters/A. Wiegmann

Kocha Joachim Loew alikuwa na mengi ya kumfaidi kufuatia mchuano huo wa kirafiki ikiwa ni pamoja na dakika 20 alizocheza nahodha Bastian Schweinsteiger baada ya kurejea kutoka mkekani, pamoja na kutofungwa bao kwa mara ya kwanza katika mechi tisa za mwisho "Kuna baadhi ya vitu tulivyofanya vizuri kuliko wiki iliyopita. Ushindi wa 2-0 unatupa hisia nzuri tunapojitayarisha kwa mpambano wa wiki ijayo. Nadhani kuna vitu tulifanya vizuri na vingine tutaimarisha wiki ijayo. Baadhi ya wachezaji wanahitaji kazi ya kufanya kwa sababu hawajawa katika hali nzuri na wanahitaji mazoezi zaidi. Lakini kwa ujumla kwa leo nimeridhishwa na maandalizi yetu kwa leo". Amesema Loew

Kiungo mshambuliaji Julian Draxler alisema baada ya pambano wa Hungary kuwa kikosi kiko tayari kwa mpambano wa kwanza "Tunajipunzisha wiki hii ili kujiweka katika hali nzuri kwa mchezo wa kwanza wa makundi. Mambo mengine, ya mbinu za kiufundi tutayajadili faraghani na tunatumai kuwa tutaonyesha uhai kwa kujituma katika mpambano wetu wa kwanza ili tushinde.

Kambi ya Ujeurumani itakuwa Evians-les-Bains ambapo mchuano wao wa kwanza utakuwa kati ya Ukraine Juni 12. Wapinzani wengine wa mabongwa hao mara tatu wa Ulaya, katika Kundi C ni Poland na Ireland Kaskazini.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Iddi Ssessanga