SiasaAsia
Ujerumani, Ufilipino kuanzisha ushirikiano wa kiusalama
4 Agosti 2024Matangazo
Kauli ya nchi hizo mbili kuhusu ushirikiano wao imetolewa wakati Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius alipotembelea Manila.
Pistorius na Waziri wa ulinzi wa Ufilipino Gilberto Teodoro, kwa Pamoja wamesema kuwa wanapinga vikali jaribio lolote la upande mmoja kuendelea na madai ya kujitanua hasa kwa kutumia nguvu au kwa kulazimisha. Hayo yanajiri wakati kukiwa na changamoto za kiusalama barani Asia, Pasifiki na Ulaya.
Makubaliano hayo ambayo huenda yakawa tayari mwezi Oktoba, yatasaidia kutanua mafunzo kati ya majeshi ya nchi hizo pamoja na ushirikano wa silaha. Ufilipino imekuwa ikitafuta ushirikiano ili kuimarisha ulinzi wakati kukiwa na mivutano inayoendelea kuongezeka kuhusu Bahari ya Kusini mwa China.