Ujerumani sasa ina serikali mpya
15 Machi 2018Mhariri wa gazeti la Rhein-Zeitung la mjini Koblenz anaandika kwamba uchaguzi mwingine wa majimbo utaonesha iwapo kile kinachoonekana kuwa ni kuaminika na wananchi kwa muungano wa vyama vya kihafidhina na SPD kuunda serikali kumefanikiwa. Mhariri anaendelea.
Mtihani wa kwanza utakuwa mnamo wakati wa kuelekea mwishoni mwa mwaka huu katika jimbo la Bavaria na kisha Hesse. Mwaka 2019 kutakuwa na mtihani mwingine wa uchaguzi wa bunge la Ulaya na kisha uchaguzi katika majimbo matatu ya mashariki mwa Ujerumani. Hali itakwenda vizuri , iwapo vyama ndugu vya CDU /CSU pamoja na SPD hadi wakati huo wataonesha kile walichofanikisha, kwamba wametatua matatizo ya wananchi.
Bila hivyo inawezekana katika majimbo ya mashariki wapiga kura watakimbilia katika chama mbadala kwa Ujerumani AfD.
Nae mhariri wa gazeti la Hannoversche Allgemeine la mjini Hannover anaandika kwamba Kansela Angela Merkel na waziri wa fedha Olaf Scholz sasa wana nafasi , kupitia sera muafaka za kubana matumizi katika sehemu kubwa ya eneo la kati nchini na kunyamazisha kile kilichoonekana kuwa ni ukweli katika majadiliano yaliyokuwapo katika miezi iliyopita. Mhariri anaandika.
Kwa mfano ni mara ngapi watu wamesikia nchini Ujerumani maneno kama "hali haiwezi kuendelea hivi" Kila mwananchi anaiangalia hali hii kwa njia tofauti. Baadhi yao ambao wanaona hali ya kiuchumi kuwa nzuri , wataendelea kupiga kura , linasema kundi linalochunguza maoni ya wapiga kura, ambao wanafikia ni karibu Wajerumani asilimia 60. Mtazamo wa wale wanaosema tuendelea hivyo hivyo kiukweli wanasema hivyo kwa misingi ya upatikanaji tu wa mahitaji ambao ndio unaowavutia zaidi.
Mzozo kati ya Uingereza na Urusi
Nalo gazeti la General-Anzeiger la mjini Bonn linaandika kuhusiana na mzozo kati ya Uingereza na Urusi kufuatia shambulio la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi nchini Uingereza. Mhariri anaandika.
Pande zote mbili zinapambana , nyuma lakini kuna hali ya kuigiza ya kutisha ambayo haieleweki. Shambulio dhidi ya jasusi wa zamani aliyeamua mwaka 2010 kukimbia kutoka Urusi haliingii akilini. Kitu kigani serikali ya Urusi itakipata kwa kufanya shambulio hilo, siku chache kabla ya uchaguzi ambao Putin anawania nchini Urusi? Kwa upande mwingine Uingereza inataka nini , kwa kufanya tukio hili ambalo si la kweli na kuweka hali ya wasi wasi kati ya Uingereza na Urusi, kama vile wanavyodai Warusi.? Hakuna, mhariri anaandika. Hali mpya mbaya ya uhusiano baridi kati ya mashariki na magharibi inaongezeka.
Mhariri wa gazeti la Stuttgerter Nachrichten akizungumzia mzozo huo kati ya Uingereza na Urusi anaandika kwamba Imegundulika hakuna ushahidi uliokwisha tolewa.Mhariri anaandika:
Kwamba waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa sauti, lakini kwa mara ya kwanza ametoa adhabu ya hovyo hovyo hivi.
Na hili hata yeye binafsi analifahamu. Kutokana na hali ilivyo Uingereza pia inabidi kuwashirikisha pia washirika. Hii inahusu Ujerumani pamoja na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya na washirika wa NATO. Kuna ishara ya wazi kwamba wote wako upande wa Uingereza, bila kujali Brexit. Na utayari , wa kuimarisha vikwazo , iwapo serikali ya Urusi itagundulika kuwa nyuma ya shambulizi hilo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Daniel Gakuba