Ujerumani, Norway zalenga robo fainali ya Kombe la Dunia
15 Juni 2015Mabingwa Japan na Brazil tayari wametinga awamu ya mchujo katika kundi C na E huku wakisalia na mechi moja ya kucheza. Na sasa mambo yatakuwa moto katika michuano ya leo Jumatatu ya Kundi A na B.
Ujerumani, mabingwa wa 2003 na 2007, wanaongoza Kundi B na pointi 4 baada ya mechi mbili, mbele ya mabingwa wa 1995 Norway ambao pia wana pointi 4. Thailand wana pointi 3, wakati Cote d'Ivoire tayari wako nje ya dimba hilo baada ya kupoteza mechi mbili.
Cote d'Ivoire watacheza leo dhidi ya Norway wakati nayo Ujerumani ikishuka dimbani na Thailand
Katika Kundi A, Canada wanaongoza na pointi 4 mbele ya China na Uholanzi walio na pointi 3 kila mmoja na New Zealand ikiwa ya mwisho na pointi moja. Canada watachuana na Uholanzi wakati China ikishuka dimbani na New Zealand
Japan ambayo tayari imefuzu katika robo fainali baada ya kuzishinda Uswisi na Cameroon katika Kundi C, sasa itapambana na Ecuador hapo kesho. Uswisi nayo itamenyana na Cameroon. Marekani inaongoza Kundi D na itamaliza kazi dhidi ya mabingwa wa Afrika Nigeria. Australia wako nyuma ya Marekani na pointi tatu na watapambana na Sweden. Alipoulizwa ikiwa wanataka kulipoza kisasi kwa kuondolewa na Sweden katika Kombe la Dunia mwaka wa 2011, mlinda mlango wa Australia Lydia Williams alisema
Timu mbili za kwanza katika kila kundi zitafuzu katika awamu ya mchujo pamoja na timu nne bora katika nafasi ya tatu kwenye makundi yote sita. Tukibalia huko Canada ni kuwa Mchezaji wa timu ya wanawake ya Nigeria Ugo Njoku amepigwa marufuku ya mechi tatu.
Kamati ya nidhamu ya FIFA imefikia uamuzi huo baada ya kutizama video inayomuonesha Njoku akimpiga kumbo mchezaji wa Australia Sam Kerr katika mechi ya makundi ya kombe la dunia la wanawake. Japo tukio hilo halikuonekana na muamuzi wa mechi hiyo, kamati hiyo ya nidhamu ilikaa na kufikia uamuzi huo pamoja na kumpiga faini ya dola elfu tatu na mia mbili.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga