Uamuzi wa kuchunguza ruzuku za China wapongezwa
13 Septemba 2023Matangazo
Ufaransa imesema Jumuiya hiyo inapaswa kutetea maslahi yake.
Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire ameuambia mkutano wa waandishi habari mjini Berlin,muda mfupi baada ya rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya,Ursula von der Leyen kutangaza hatua hiyo,mbele ya bunge la Ulaya,mjini Strassburg,kwamba kuanzishwa kwa uchunguzi huo ni uamuzi mzuri sana.
Ujerumani kupitia waziri wake wa uchumi, Robert Habeck imesema uchunguzi dhidi ya ruzuku inayotolewa na serikali ya China,unaonesha mwelekeo mzuri wa Umoja wa Ulaya na unahusu zaidi kutafuta suluhu ya ushindani usiokuwa wa haki.