1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani mwenyekiti wa G20

Jane Nyingi
1 Desemba 2016

Ujerumani imetwaa uwenyekiti wa kundi la G20.Hayo yanajiri wakati ambapo kuna wasiwasi na dalili kuwa ushirikiano wa nchi za magharibi unakabiliwa na changamoto kubwa tangu vita vikuu vya pili vya dunia.

https://p.dw.com/p/2TbH9
China G20 Gipfel in Hangzhou - Angela Merkel
Picha: Reuters/E. Oliveau

Tayari serikali ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel imeweka wazi ajenda yake inapochukua uongozi wa kundi hilo. Miongoni mwa yaliyomo katika agenda hiyo ni pamoja na  kulenga biashara ya kimataifa na kuendelea na malengo yake katika swala la mabadiliko ya tabia nchi. Swala lingine ni kushughulikia tishio  linalotokana na ongezeko la siasa  kali za kizalendo. Chini ya kauli mbiu kuchagiza dunia iliyounganishwa,uongozi wa G20 wa Merkel pia unataka kundi hilo kuangazia zaidi bara la Afrika na pia kuendelea kupambana na wanaokwepa kulipa kodi, huku  likiendeleza kanuni za  ukuaji wa soko la kimataifa.
Hii ni mara ya kwanza Ujerumani  kuchukua uwenyekiti  wa kundi la G20,ambalo linawakilisha zaidi ya asimilia 80 ya shughuli za kiuchumi duniani na kujumuisha mataifa yayoendelea zaidi kiuchumi.Waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schaeuble akizungumzia kuhusu kumalizika uwenyekiti wa china  katika kundi hilo la G20 alisema“Maandalizi ya kutoa uwenyekiti  yangekuwa magumu zaidi bila ya ushirikiano wa karibu.Tulifaidika kwa mengi kutokana na uwenyekiti uliotangulia wa China.Tutajaribu kuendelea bila hiana na kazi hii kwa sababa nguvu za kundi la G20 zinaendelea chini ya kila uongozi unoaingia."Kansela Angela Merkel anatarajia kwamba  uwenyekiti wa nchi yake utakuwa ni nafasi mwafaka kwake kuonyesha uwezo wake katika jukwaa la siasa za dunia kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu hapa Ujerumani  mwezi Septemba mwaka ujao. Akizungumza hivi karibuni Kansela Merkel amepuuza ukosoaji wa mikutano mikubwa kama ya kundi la G20 akisisitiza kwamba kuwa chombo hicho kinaendelea kubeba dhima muhimu.Hata hivyo kwa upande mwingine agenda za Merkel katika kundi hilo la G20 huenda zakatatizwa na ahadi za rais mteule wa Marekani Donal Trump za kutaka kuilinda nchi yake. Si hilo tu lakini pia kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ni hatua ambayo imewatia mashaka  wanasiasa wengi kuwa ongezeko la viguvugu la siasa za kizalendo huenda pia zikaota mizizi Ulaya.Kwa upande wake Trump ameshaonyesha ishara kwamba ana mipango ya kuchukua mkondo tofauti katika maswala ya dunia na ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Barack Obama. Kadhalika  mkutano kilele wa  viongozi wa kundi hilo la G20  huenda ukaenda sambamba na kuanzishwa rasmi kwa mchakato wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya  utakaoanzishwa na waziri mkuu Theresa May.

Florida Trump-Anhänger David Ramirez
Wafuasi wa rais mteule wa Marekani Donald TrumpPicha: picture-alliance/ZUMAPRESS
Deutschland Auftakt der deutschen G20-Präsidentschaft 2017
Waziri wa fedha Wolfgang SchäublePicha: picture alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Mkutano huo utakaofanyika mjini Hamburg hapa Ujerumani na kuongozwa na Kansela Maerkel pia utahudhuriwa  na rais Urusi Vladmir Putin ambae hadi wakati huu amekuwa akijikuta ametengwa na jumuiya ya kiamataifa kutokana na hatua ya serikali yake kuwaunga mkono waasi mashariki mwa Ukaraine pamoja na kunyakua kimabavu rasi ya Kremia iliyokuwa chini ya Ukraine.Wakati huo huo wachambuzi wa mambo wanahisi kwamba wasiwasi  unaotokana na majadiliano ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya pamoja na mashaka  kuhusiana na mipango isiojulikana na Marekani chini ya Trump ni mambo yanayoweza kuongeza vitisho katika mustakabali wa  hali ya kiuchumi duniani.

Mwandishi:Jane Nyingi/DPA
Mhariri: Daniel Gakuba