Ujerumani: Mashambulizi ya mtandao kutoka nje yameongezeka
13 Mei 2024Kulingana na data hiyo mpya, mashambulizi ya mtandaoni yanatoka hasa Urusi na China.
Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kitaifa kuhusu uhalifu wa mtandao, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser amesema, ''kiwango cha kitisho mtandaoni kinasalia kuwa juu.''
Hili ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo mashambulizi ya mtandaoni yaliongezeka kwa asilimia nane.
Kuna wasiwasi mkubwa juu ya washukiwa wa udukuzi na majasusi wakati huu wa maandalizi ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya. Na chama cha sekta ya kidijitali cha Ujerumani, Bitkom kiliripoti kuongezeka maradufu kwa idadi ya mashambulizi ya mtandao kutoka Urusi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Uharibifu wa kiuchumi unaosababishwa na uhalifu wa mtandaoni huigharimu Ujerumani euro bilioni 148 bilioni kwa mwaka.