Ujerumani kuumana na Ukraine
10 Juni 2016Ujerumani watacheza kesho Jumapili dhidi ya Ukraine katika Kundi C, ambalo pia lina mpambano kati ya Poland na Ireland ya Kaskazini. Licha ya wasiwasi wa majeruhi ya hapa na pale kikosini, Ujerumani wako tayari kuanza safari yao ya kutafutwa ubingwa wa Ulaya. Manuel Neuer ni kipa wa die Mannschaft "Nadhani tuna furaha kuwa dimba hatimaye linaanza. Tumekuwa na muda wa maandalizi na mafunzo tunayohitaji na sasa michuano yenyewe inaanza. Tuna furaha kucheza mechi yetu na Ukraine Jumapili. bila shaka tutaangalia trelevisheni na kuona tulivyocheza. Hisia kambini ziko sawa kabosa na tunasubiri tu kushuka dimbani sasa.
Kuna maswali katika safu ya ulinzi ya Ujerumani wakati kocha Joachim Loew anasubiri kuona ikiwa Mats Hummels atakuwa katika hali nzuri kucheza. Benedict Hoewedes huenda akapangwa pamoja na Jerome Boateng, lakini licha ya yule atakayechaguliwa, Wajerumani wana matumaini kuwa watakuwa sawa tu. Jonas Hector ni beki wa Ujerumani "Unaweza kusema ni kitu kingine kabisa inapokaribia michuano ya ubingwa wa Ulaya. Bila shaka nnajihisi vizuri lazima nikiri hilo. Natamani sana michezo kuanza, na tena kuwa hapa kwa wiki nne au tano, hivyo tunataraji tutakuwa hadi Julai 10. Ni maarifa mapya kuwa pamoja na nafurahia wakati huu.
Mpambano mwingine wa Uturuki dhidi ya Croatia mjini Paris utakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwa sababu huenda ikaamua timu itakayoshika nafasi ya pili katika Kundi D nyuma ya mabingwa watetezi wa Ulaya Uhispania.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef