Ujerumani kushiriki katika vita Afghanistan
23 Julai 2009Tangu mwanzoni mwa wiki hii kumekuwa na mapambano dhidi ya kundi la Taliban kaskazini mwa Afghanistan, na jeshi la Ujerumani Bundeswehr linashiriki katika mapambano hayo. Hadi hivi karibuni wanajeshi wa Ujerumani walikuwa tu wakifanya mashambulio ya kujihami. Hivi sasa binafsi wako vitani , na wanatumia silaha kali kama vile makombora, na vifaru. Waziri wa ulinzi Franz-Josef Jung ametetea hatua hiyo mjini Berlin kwa kueleza kuwa hali imekuwa mbaya katika jimbo la Kunduz. Wapiganaji katika eneo hilo wamekuwa wakifanya mashambulio ya kushtukiza mara kwa mara.
Sio hatua ya kivita, ameeleza waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz-Josef Jung katika mkutano na waandishi habari. Wanajeshi wa Bundeswehr wako chini ya uongozi wa jeshi la kimataifa la ISAF, na mashambulio wanayofanya yanaongozwa na jeshi la Afghanistan. Pamoja na wanajeshi 300 wa Ujerumani, wako wanajeshi 800 wa Afghanistan pamoja na polisi 100 wa Afghanistan ambao wanahusika katika operesheni hiyo.
Kuhusiana na swala iwapo matumizi ya silaha kali kwa jeshi la Ujerumani ni aina mpya ya kiwango cha ubora, anaeleza mkuu wa kikosi hicho , inspekta jenerali Wolfgang Schneiderhan.
Hakuna haja ya kuongezwa wanajeshi. Hakuna hali iliyobadilika. Kwa kuwa changamoto za tangu karibu mwezi wa March kupitia mbinu tofauti zinaendelea kuwapo, na ongezeko la mashambulio ya mabomu dhidi ya jeshi ni hali iliyozoeleka.Ndio sababu kumekuwa na haja ya kukitumia kikosi cha kuchukua hatua za haraka ama kile cha ziada ili kuweza kuzuwia hali hii.
Kutoka upande wa upinzani hata hivyo kunatolewa sauti za tahadhari. Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kutoka katika chama cha ulinzi wa mazingira katika bunge la Ujerumani, Wilfried nachtweih, amesema katika radio ya mjini Berlin, kuwa ingewezekana kuwazuwia Taliban katika jimbo la Kunduz, iwapo jeshi la polisi la Afghanistan lisingepunguzwa. mashambulio ya hivi sasa ni jibu na yatakuwa ya hatari, anasema Nachtweih.
Huu utakuwa ni mzunguko usiokwisha, na hapa tunapaswa kuchukua tahadhari ya juu kabisa, kwamba tusijiingize katika hatua ya kuongeza machafuko zaidi bila kujua mwishowake.
Kwa upande mwingine jenerali Schneiderhan anaamini kuwa kutapatikana mafanikio katika mashambulio haya. Na sababu ikiwa ni kutokana na uchaguzi mkuu wa Afghanistan uliopangwa kufanyika katika muda wa siku 30.
Kile tunachokifanya kwa wakati huu, ni kuweza kupata uimara na kuweka usalama na kuwa na hali ya utulivu wakati wa uchaguzi katika jimbo pia la Kunduz. Na hii inaonekana kuwa kinaweza kuwa ni kikwazo.
Waziri wa ulinzi Franz Josef Jung ameeleza kuwa lengo la jeshi la Ujerumani katika operesheni hii nchini Afghanistan ni kuiondoa nchi hiyo katika hali ya sasa ya mapigano ili nchi hiyo iweze kujilinda binafsi.
Wakati ninajikuta katika hali fulani , nikiwa na maana ya operesheni ya hivi sasa katika jimbo la Kunduz, kama jeshi la Afghanistan linavyofanya , kwa hiyo naweza kusema, kwa mtazamo wangu mambo yanakwenda vizuri.
Hatua pia zinapingwa katika ujenzi mpya. Kiasi cha watoto wanaofikia milioni 6.5 wanakwenda shule tena nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja na wasichana , kuna vyuo vikuu 19, asilimia 85 ya wananchi wanapata matibabu, ameeleza waziri Jung.
Mwandishi: Stützle, Peter/Kitojo, Sekione
Mhariri: Josephat Charo