1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kurefusha muda wa viwanda vya nyuklia

30 Agosti 2010

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,anataka kurefusha muda wa viwanda vya nishati ya nyuklia kwa hadi miaka kumi na tano. Amesema, kiufundi huo ni muda unaoingia maanani, kwa kuzingatia ripoti ya wataalamu.

https://p.dw.com/p/Oz6t
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) gibt am Donnerstag 26. August 2010, nach einem Besuch des Kernkraftwerks in Lingen, Niedersachsen, ein Statement ab. Sie traf sich zuvor mit Bundesumweltminister Norbert Roettgen (CDU), Juergen Grossmann, Vorstandsvorsitzender des Energieversorger RWE, Johannes Teyssen, Vorstandsvorsitzender des Energieversorgers E.ON. (apn Photo/Joerg Sarbach) ---- German Chancellor Angela Merkel (CDU) gives media a statement after a visit in the nuclear power plant in Lingen , Germany, on Thursday, Aug. 26, 2010.(apn Photo/Joerg Sarbach)
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha nishati ya nyuklia cha Lingen, Ujerumani.Picha: AP

Hata hivyo,ni lazima kuhakikisha usalama wa viwanda hivyo vya nyuklia. Kwa maoni yake, utaratibu wa kurefusha muda wa viwanda hivyo, uandaliwe kwa njia ambayo hautohitaji kuidhinishwa na baraza la waakilishi wa serikali za majimbo "Bundesrat."

Baadhi ya majimbo yanayoongozwa na chama cha kisoshalisti cha SPD yametishia kuifikisha kesi hiyo katika mahakama ya katiba. Kiongozi wa SPD, Sigmar Gabriel amemtuhumu Merkel kuridhia sera za washawishi wa kampuni za nishati ya nyuklia. Amesema, kwa kukutaka kurefusha muda wa viwanda hivyo, Kansela Merkel anauza usalama wa umma. Hata chama cha mazingira cha Kijani na Die Linke cha mrengo wa kushoto vimemkosoa Merkel.

Der SPD Vorsitzende Sigmar Gabriel verfolgt beim SPD Parteitag am Sonntag, 15. November 2009 in Dresden, Sachsen, die Debatte. Der SPD Parteitag findet vom 13.11. bis 15.11.2009 statt. (AP Photo/Markus Schreiber)-----SPD party leader Sigmar Gabriel listens to the debate during the party congress of Germany's Social Democrats, SPD, in Dresden, Germany, Sunday, Nov. 15, 2009. The SPD holds their party congress in Dresden from Friday, Nov. 13, to Sunday, Nov. 15, 2009. (AP Photo/Markus Schreiber)
Mwenyekiti wa chama cha SPD, Sigmar Gabriel.Picha: AP

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,anataka kurefusha muda wa viwanda vya nishati ya nyuklia kwa hadi miaka kumi na tano.Amesema, kuambtana na ripoti ya wataalamu, kiufundi, huo ni muda unaoingia maanani.

Hata hivyo, usalama wa viwanda hivyo vya nyuklia unapaswa kuhakikishwa.Kwa maoni yake,utaratibu wa kurefusha muda wa viwanda hivyo, uandaliwe kwa njia ambayo hautohitaji kuidhinishwa na baraza la waakilishi wa serikali za majimbo "Bundesrat."

Baadhi ya majimbo yanayoongozwa na chama cha kisoshalisti cha SPD yametishia kuifikisha kesi hiyo katika mahakama ya katiba. Kiongozi wa SPD, Sigmar Gabriel amemtuhumu Merkel kuridhia sera za washawishi wa kampuni za nishati ya nyuklia. Amesema, kwa kukutaka kurefusha muda wa viwanda hivyo, Kansela Merkel anauza usalama wa umma. Hata chama cha mazingira cha Kijani na Die Linke cha mrengo wa kushoto vimemkosoa Merkel.

Mwandishi/P.Martin/ZPR