1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kupepetana na England

Yusra Buwayhid
24 Juni 2021

Ujerumani ilikuwa hatarini kutolewa kwenye michuano ya kuwania ubingwa wa Ulaya katika Kundi F Jumatano hadi pale Leon Goretzka alipofyatua bao na kuipatia timu yake sare ya mabao mawili dhidi ya Hungary.

https://p.dw.com/p/3vTdS
Fußball EM EURO 2021 | Deutschland v Ungarn Torjubel
Picha: Lukas Barth/epa/dpa/picture alliance

Timu hiyo inayoongozwa na kocha Joachim Löw sasa imefuzu hatua ya 16 bora katika michuano hiyo ya mataifa ya Ulaya.

Mlinda mlango wa Ujerumani Manuel Neuer alisema mchezo wao dhidi ya Hungary ulikuwa mgumu na wenye kusisimua.

Hungary ilitawala kipindi cha kwanza cha mechi hiyo iliyochezwa mjini Munich Ujerumani.

Fußball EM EURO 2021 | Deutschland v Ungarn Tor Goretzka
Leon Goretka akipachika wavuni goli la pili la UjerumaniPicha: Christian Charisius/dpa/picture alliance

Wembley kuwa mwenyeji wa Ujerumani na England

Kai Havertz wa Ujerumani alifunga goli la kwanza katikakipindi cha pili cha mchezo baada ya Hungary kuingia uongozini kupitia kwa nahodha wao Adam Szalai. Lakini dakika mbili baadae Hungary iliongeza la pili lilofungwa na Andras Schäfer. Na hapo ndipo Goretzka alipokuja kuiokoa timu yake ya Ujerumani na kuipatia sare ya mabao mawili dakika sita kabla ya mechi kumalizika.

Wiki ijayo siku ya Jumanne, Ujerumani itakabiliana na England mjini London katika uwanja wa Wembley zitakapochuana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali.

Kocha wa Ujerumani Löw amekiri kwamba timu yake ilifanya makosa mengi ilipocheza na Hungary, lakini ameapa kuwa watacheza mchezo bora zaidi dhidi ya England wiki ijayo.

England ilipoteza mikwaju ya penati

Haitakuwa mechi ya kawaida kwani England itakuwa inajaribu kulipiza kisasi  kutokana na kipigo walichopewa na Ujerumani katika nusu fainali ya michuano ya Ulaya ya mwaka 1996 kwenye uwanja huo huo wa Wembley.

Deutschland München | UEFA EURO 2020 | Portugal vs Deutschland | Joachim Löw
Kocha wa Ujerumani Joachim LöwPicha: Philipp Guelland/AFP/Getty Images

England ilifungwa kupitia mikwaju ya penati, na Ujerumani ikasonga mbele na kuchuana katika fainali na Jamhuri ya Czech na kunyakuwa ushindi wa kombe la Ulaya mwaka 1996.

Mechi nyingine zilizochezwa Jumatano ni Ureno dhidi ya Ufaransa zilizotoka sare ya mabao mawili. Uhispania iliifunga Slovakia mabao 5-0 na Sweden ikaibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Poland.