1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani Kufanya mageuzi ya kisheria kwenye familia

22 Februari 2024

Ujerumani inakabiliwa na idadi ya watu wanaozeek na watu wanaoishi peke yao, serikali inapanga kuanzisha utaratibu mpya wa kisheria na kuwasaidia wale ambao wapo kwenye mahusiano kuwajibika kila mmoja.

https://p.dw.com/p/4cZc0
Familia ikiwa katika mlo wa pamoja
Familia ikiwa katika mlo wa pamojaPicha: Monkey Business 2/Shotshop/IMAGO

Jinsi watu wanavyoishi, mapenzi, uzazi na umri nchini humo vinabadilika. Lakini suala la nani na jinsi ya kutunza mtu mwingine iwe utunzaji wa watoto au kutunza wazee bado ni kubwa katika jamii ambayo mmoja kati ya watu wanne wanasema ni wapweke. 

Ikitajwa na waziri wa sheria Marco Buschmann kama mageuzi ambayo huenda yakawa makubwa zaidi ya sheria ya familia katika miongo kadhaa, msingi wa pendekezo moja linalowezekana kuwa la kiitikadi  sasa limekubaliwa na serikali ya mseto ya Ujerumani ya chama cha Social Democratic SPD, Greens na Free Democratic FDP.

Kile kinachotajwa kuwa jamii ya uwajibikaji ni kutoa utaratibu mpya wa kisheria ambao vikundi vya kati ya watu wawili hadi sita vitaweza kuchukua jukumu la kisheria kwa kila mmoja, kwa mfano katika kesi ya dharura ya matibabu.

Soma pia:Joto lahusishwa na vifo vya watu 3,100 Ujeumani

Andrea Newerla, mwanasosholojia ambaye amefanya utafiti kuhusu mifumo ya mapenzi na mahusiano anasema ukweli ni kwamba hakuna usalama katika mahusiano ya kimapenzi ya kisasa na mara nyingi watu hujifunza hilo kupitia hali ngumu.

Katika jamii yenye watu wengi wanaozeeka, Newerla anasema suala la jinsi tunavyotaka kuishi pamoja na usaidizi ambao watu wanategemea linahitaji kufikiriwa upya kabisa.

Newerla anaelezea mfano wa familia zilizoundwa na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kwa sababu ya kukataliwa na familia zao za kibaolojia baada ya kujieleza kuwa hivyo, na kwamba maisha yetu ya kila siku labda yangekuwa na mpangilio mzuri zaidi kwa kuzingatia urafiki tofauti na ushirika wa kimapenzi.

Mfumo kurahisishia maisha wazee, wanao leo watoto peke yao

Serikali inasema kwamba jamii ya uwajibikaji itasaidia kurahisisha maisha kwa wazee na wazazi wasio na wenzi. Hata hivyo, makundi ya kutetea haki yanatilia mashaka kuhusu kiasi cha tofauti itakayoleta katika maisha ya watu.

Mhudumu akimsaidia mzee kutembea katika eneo la kubarizi kwenye bustani.
Mhudumu wa wazee, akimsaidia mzee kutembea katika eneo la kubarizi kwenye bustani.Picha: Kasper Ravlo/Zoonar/IMAGO

Regina Gorner, mwenyekiti wa chama cha kitaifa cha mashirika ya wazee BAGSO, ameiambia DW kwamba hafikirii kutakuwa na mabadiliko makubwa kwa wazee na kwamba kuna mikakati ambayo tayari imewekwa kama vile hati za kuthibitisha mtu atakayekuwa na jukumu la kumfuatilia mgonjwa na pia kumfanyia maamuzi ambazo hazina urasimu mwingi.

Wazee wana uwezekano wa kuishi peke yao mara mbili zaidi kuliko idadi ya watu wa kawaida.Takriban asilimia 32 ya watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi katika Umoja wa Ulaya waliishi peke yao mwaka wa 2022, nchini Ujerumani idadi hiyo ilikuwa asilimia 34, kulingana na Taasisi ya Kisayansi ya Chama cha Bima Binafsi za Afya (WIP).

Soma pia:Kansela Scholz kulihutubia Bunge kuhusiana na matatizo ya bajeti

Taasisi hiyo inatabiri kuwa hadi watu milioni 5.75 watahitaji huduma nchini Ujerumani ifikapo 2030.

Heidi Thiemann, mwanzilishi wa Alltagsheld:innen, taasisi inayotetea haki za wazazi wasio na wenzi wa ndoa, anaelezea hali kama hiyo.

Thiemann ameiambia DW kwamba wazazi wasio na wenzi wa ndoa wanahitaji vitu tofauti sana ili kuweza kuboresha hali zao. Ameongeza kwamba kile kinachozungumziwa ni kwamba hilo ni chaguo ambalo hakuna aliyeliomba. 

Ukosoaji wa mageuzi hayo pia umetoka kwa chama cha upinzani cha Christian Democrats (CDU/CSU) na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha  (AfD).

Msemaji wa sera ya sheria wa CDU Günter Krings alipendekeza kuwa utaratibu mpya wa kisheria unaweza kufungua njia kwa wanaume kuoa wake wengi  ambayo kwa sasa inatambulika nchini Ujerumani kwa ndoa za aina hiyo zilizofungwa kisheria nje ya nchi.

Newerla angependa kuona aina mpya zinazoendelea na za majaribio za ujumuishaji na umoja zikiungwa mkono na serikali, lakini ana wasiwasi kuwa hali ya sasa ya kisiasa barani Ulaya inaenda kinyume na hayo.

Ushirikiano wa matibabu ya kibingwa kati ya Ujerumani- Kenya