Ujerumani bado yashinikiza kuachana na nishati visukuku
7 Desemba 2023Matangazo
Berbock amesema hayo kabla ya kuondoka kwenda kuhudhuria mkutano huo. Amesema Ujerumani itapania kwenye mkutano huo na itafanya kila kitu ikiwa lazima, kwa ajili ya lengo hilo. Berbock ameeleza kuwa dunia inahitaji makerebisho. Amesema ili kufikia lengo la kupunguza joto la dunia, hadi nyuzi joto 1.5, pana ulazima wa kuongeza uzalishaji wa nishatiendelevu mara tatu ifikapo mwaka 2030. Kwenye mkutano huo wa Dubai washiriki zaidi ya 100, ikiwa pamoja na kutoka Umoja wa Ulaya na Marekani wameahidi kuchukua hatua za kuelekea kwenye lengo la kuondosha nishati za visukuku hatua kwa hatua.