Ujerumani inaadhimisha miaka 33 tangu kuungana tena kwa pande mbili za mashariki na magharibi ambazo zilitengana muda mfupi baada ya kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia. Saumu Njama amezungumza na mwandishi wa zamani wa DW na mchambuzi wa siasa za kimataifa Abdul Mtulya na kwanza amemuuliza je kuna mabadiliko yoyote tangu wakati huo?