SiasaUingereza
Uingereza yasema inaisaidia Israel kuwatafuta mateka
3 Desemba 2023Matangazo
Katika tangazo lake la jana jioni, serikali hiyo imesema kuwa kwa kuunga mkono operesheni hiyo ya kuwaokoa mateka wa Israel, wizara ya ulinzi ya Uingereza itapeleka ndege zake za ufuatiliaji Mashariki mwa Mediterenia pamoja na anga ya Israel na Gaza.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa ndege hizo za ufuatiliaji hazina silaha na hutumika kutambua maeneo ya mateka na kwamba habari za pekee zinazohusiana na uokoaji wa mateka hao, zitawasilishwa kwa mamlaka husika.
Takriban watu 240 walitekwa nyara na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas wakati wa uvamizi wa kushtukiza dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7 mwaka huu.