Mpango wa ujenzi wa ukuta mkuu huko Calais nchini Ufaransa kuwadhibiti wakimbizi na wahamiaji wanaokimbilia Uingereza unazusha hofu ya kuifanya Ulaya kuwa bara lisiloingilika. Zaidi ya wakimbizi 6,000 wanaishi kwenye mazingira duni katika kambi ya Calais.