Uingereza kuhamisha tembo hadi Kenya
6 Julai 2021Matangazo
Wakfu huo umesema utatumia masanduku yaliyotengenezwa maalum kuwafungia Tembo hao ndani ya ndege aina ya Boeing 747 watakapokuwa wakisafirishwa.
Jumla ya tembo 13 aina ya Pachyderms kwa lugha ya Kiingereza watahamishwa kutoka mazingira yao ya sasa karibu na Canterbury kusini mashariki mwa England.
Maafisa wa wakfu huo wamesema, mradi huo ambao umepangwa kufanyika mwaka ujao, utakuwa wa kwanza wa kuhamisha ndovu katika mazingira tofauti.
Mkuu wa idara ya mawasiliano katika wakfu huo ambaye pia ni mke wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema mpango huo pia utasidia kuimarisha uchumi wa Kenya baada ya janga la virusi vya corona.