Uingereza kuanzisha mazungumzo ya kibiashara na Korea Kusini
21 Novemba 2023Mkataba huo mpya wa biashara huria utachukua nafasi ya mkataba uliopo sasa ambao kwa kiasi kikubwa, una vipengee vilivyokuwepo hata kabla ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.
Ziara ya Yoon inaanza rasmi leo ambapo atakaribishwa na Mfalme Charles, kwa kupewa heshima kuu za kijeshi na kuandaliwa karamu katika kasri la Buckhingham, kuashiria ziara ya kwanza ya serikali iliyoandaliwa na Uingereza tangu kutawazwa Charles kuwa mfalme.
Yoon, mhafidhina ambaye ametaja changamoto nyingi za kimataifa kama sababu ya kutafuta uhusiano wa karibu na washirika wenye fikra sawa , pia atahutubia mabunge yote mawili ya Uingereza, kabla ya kufanya mazungumzo na Sunak juu ya biashara, teknolojia na ulinzi.
Kupitia taarifa Sunak ameeleza kuwa, makubaliano kati ya Uingereza na Korea Kusini yatachochea uwekezaji, kukuza biashara na kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.