Uingereza imeanza kubana uhuru wa vyombo vya habari?
30 Oktoba 2013Mwandishi wetu Regina Menning anasema katika taarifa yake kwamba Uingereza inaelekea katika mkondo wa kuubana uhuru wa vyombo vya habari kwa kisingizio cha kuulinda usalama wa taifa.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliufafanua msimamo huo kandoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Brussels hivi karibuni. Alipozumzia juu ya adui, Waziri Mkuu Cameron alikuwa na maana ya Edward Snowden wakala wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani ka NSA aliefichua siri za shirika hilo. Kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Cameron vyombo vya habari, kama gazeti la "Guardian "pia ni adui wa harakati za kupambana na ugaidi .
Mwandishi wa gazeti hilo Glenn Greenwald alizichapisha habari za kwanza za siri alizopewa na aliekuwa mfanyakazi wa shirika la ujasusi la Marekani la NSA, Edward Snowden. Waziri Mkuu wa Uingereza ametoa vitisho dhidi ya gazeti la "Guardian" Na siyo yeye peke yake.
Kwa muda wa wiki kadhaa sasa vyombo vya habari muhimu nchini Ungereza vimekuwa vinalisakama gazeti la Guardian. Vyombo hiyvo vinesema katika tahariri kali kwamba kwa kukubali kuzichapisha siri zilizofichuliwa na Edward Snowden, gazeti hilo limewasaida maadui wa Uingereza. Kiongozi wa maripota wasiojali mipaka tawi la Ujerumani Michael Rediske amesema vitisho kama hivyo ni jambo lisilowezekana nchini Ujerumani.Amekumbusha juu ya mzigo wa historia unaobebwa na wajerumani.
Nchini Ujerumani watu wanakumbuka yaliyotokea wakati wa utawala wa mafashisti.Dhana kama maslahi ya kitaifa au siri za nchi zilitumika kama sababu. Katika baadhi ya nchi, miongoni mwao ,Uingereza vitabu vya sheria vinatumiwa kuimarisha ulinzi wa siri za nchi."
Mkuu huyo wa waandishi wa tawi la Ujerumani la waandishi wa habari wasiojali mipaka bwana Rediske amesema vyombo vya habari nchini Ujerumani vina makucha ya kuwaewzesha kujitetea.Ametoa mfano wa alieyekuwa Rais wa Ujerumani, Christian Wulff aliejaribu kumtisha mhariri mkuu wa gazeti la "Bild.
Rais huyo wa zamani alimpigia simu mhariri huyo ili kujaribu kuzuia kuchapishwa kwa taarifa juu ya mkopo uliokuwa na utata aliopewa bwana Wulff. Mkasa huo ulitifua tufani iliyomng'oa madarakani Rais huyo. Lakini serikali ya Uingereza inavishinikiza vyombo vya habari kwa kisingizio cha usalama wa taifa. Hata hivyo mwakilishi wa waandishi habari wasiojali mipaka bwana Rediske amesema inapasa kutilia maanani kwamba magaidi waliwahi kufanya mashambulio mabaya katika treni ya chini ya ardhi nchini Uingereza.
Mwandishi:Menning, Regina
Tafsiri:Mtullya Abdu
Mhariri: Yusuf Saumu