Uhusiano wa nchi za Afrika na Ujerumani ya Mashariki
Ujerumani ya Mashariki ilitafuta uhusiano na mataifa ya Kiafrika kama vile Angola, Ethiopia, Msumbiji na Tanzania. Lakini uhusiano ulimalizika baada ya kuungana tena Ujerumani ya Mashariki na Magharibi miaka 25 iliyopita
Mafunzo ya ufundi
Wafanyakazi wenye ujuzi kutoka nchi za Kiafrika zilizokuwa na siasa za kijamii za Marxist na Leninist, walipata mafunzo ya ufundi Ujerumani ya mashariki ambayo ilikuwa na siasa za kikomunisti hadi pale ilipoungana tena na Ujerumani ya Magharibi Oktoba 3, mwaka 1990. Waangola hawa walikuwa wakipata mafunzo ya miezi sita katika Taasisi ya Usalama wa Viwanda mjini Dresden.
Harakati za ukombozi wa nchi za Afrika
Ndege iliyokuwa ikimilikiwa na shirika la Ujerumani ya Mashariki Interflug ikiwa imetuwa katika uwanja wa ndege wa Luanda nchini Angola, Ilibeba vifaa vya shule. Walengwa wengine wa Kamati ya Mshikamano ya Ujerumani ya Mashariki mwaka 1978, ni Chama cha ukombozi cha Zimbabwe (ZANU), chama cha ukombozi wa Namibia (SWAPO), pamoja na chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC).
Mafunzo kwa waandishi habari
Ujerumani ya Mashariki ilitoa mafunzo kwa mamia ya waandishi habari kutoka kila kona ya bara la Afrika. Walihudhuria 'Shule ya Mshikamano' iliyokuwa ikiendeswa na Shirikisho la Waandishi Habari la Ujerumani ya Mashariki. Mafunzo hayo waliyopewa waandsihi habari kutoka nchi kama Guinea-Bissau, Cape Verde na Sao Tome na Principe yalifanyika Disemba mwaka 1976.
'Shule ya Urafiki'
Margot Honecker, waziri wa elimu na mke wa Kiongozi Mkuu wa Ujerumani ya Mashariki Erich Honecker, akiwa anasalimiana na Samora Machel, Rais wa kwanza wa Msumbiji wakiwa katika Shule ya Urafiki mjini Straßfurt mwaka 1983. Msumbiji na Ujerumani ya Mashariki walikubaliana mwaka 1979 kwamba wanafunzi 899 kutoka Msumbiji watahudhuria shule hiyo ya Ujerumani ya Mashariki kwa muda wa miaka minne.
Shule ya Sekondari ya Dr Agostinho Neto
Rais wa Angola Eduardo dos Santos akiwa ziarani Ujerumani ya Mashariki. Wanachama wa tawi la vijana la chama cha kikomunisti cha Ujerumani ya Mashariki, FDJ, walimpokea rais wa Angola huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa “Upande wa Umoja wa Kisovieti, kwa amani na ujamaa!”
Rais wa Angola akiwa katika ukuta wa Berlin
Rais wa Angola dos Santos pia aliutembelea ukuta wa Berlin ulioko mbele ya lango la Brandenburg, Berlin ya Mashariki. Ujerumani ya Mashariki ilijenga ukuta huwo kuitenga Ujerumani ya Magharibi Agosti mwaka 1961, ili kuwazuia Wajerumani wa Mashariki wasikimbilie upande wa Magharibi. Ujerumani ya Mashariki iliuita ukuta huwa kuwa ni "kizuizi dhidi ya ufashisti".
Mkutano wa Chama cha Kikomunisti
Chama tawala cha kikomunisti cha Ujerumani ya Mashariki (SED) kikiwakaribisha wageni kutoka nchi za nje wenye itikadi za kisiasa zinazolingana na zao katika mikutano yao. Miongoni mwa wageni wa mwaka 1981 ni Ambrosi Lukoki, mwanachama wa chama cha MPLA kutoka Angola, pamoja na Berhanu Bayeh (mstari wa mwisho wapili kutoka kushoto), waziri wa nje wa Ethiopia wakati wa uongozi wa kidikteta wa Derg.
Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Ujerumani ya Mashariki (SED)
Viongozi wa ngazi za juu wa Kiafrika wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto za Ki-Marxist na Leninist waliitembelea Ujerumani ya Mashariki na wenzao wa Ujerumani Mashariki waliitembelea Afrika. Mwanachama wa politburo wa Ujerumani Mashariki Konrad Naumann, alihudhuria mkutano wa tatu wa chama cha Afrika kwa ajili ya Uhuru wa Guinea na Cape Verde (PAIGC) nchini Bissau mwezi Novemba mwaka 1977.
Watoto wa shule wa Ujerumani ya Mashariki na wa Afrika
Kasumba za ´kikomunisti kwa watoto wa shule wa Ujerumani Mashariki ziliendelea hata wakati wa likizo ambapo walihudhuria kambi za vikundi vya viajana vya Young Pioneers and Thälmann Pioneers . Mgeni huyu kutoka Jamhuri ya Watu Kongo anaoneshwa gazeti la Die Trommel, la kikundi cha Thalmann mjini Berlin ya Mashariki.
Wikiendi na familia ya Ujerumani ya Mashariki
Vijana wa Kiafrika waliohudhuria kambi ya majira ya joto ya mwaka 1982 ambao walifikia katika familia za Ujerumani Mashariki kwa wikiendi nzima. Treni maalum iliwapeleka Schwedt, mji wa viwanda karibu na mpaka na Poland. Sandra Maria Bernardo kutoka Angola akiwa anakaribishwa na mwenyeji wake Ingeborg Scholz na binti yake Petra.
Matrekta kwa "Udugu wa mataifa ya siasa za ujamaa"
Mwaka 1979 kiwanda cha matrekata cha Ujerumani ya Masharikimjini Schönebeck kiliifadhili Ethiopia matrekta kadhaa lilipokuwa taifa la itikadi kali za mrengo wa kushoto za Ki-Marxist na Leninist. Matrekta hayo ya chapa ya ZT 300-C yalisafirishwa kwenda nchi 26, ikiwa ni pamoja na Angola na Msumbiji.
Mashine za kutengenezea nguo Ethiopia
Kiwanda hiki cha nguo kilichopo Kombolcha katika jimbo la Ethiopia la Amhara (picha: Novemba 2005) kinazalisha shuka na taulo. Kilijengwa mwaka 1984 kwa msaada wa Ujerumani ya Mashariki na Chekoslovakia (sasa Jamhuri ya Czech na Slovakia). Karibu mashine zote zilitengenezwa na kiwanda cha combine TEXTIMA mjini Karl-Marx-Stadt (sasa Chemnitz).
Majengo ya 'Michenzani' visiwani Zanzibar
Muasisi wa taifa laTanzania ni Julius Nyerere mwaka 1964. Na Ujerumani ya Mashariki ilimsaidida Nyerere katika kuanzisha siasa za Ujamaa nchini humo kwa kujenga majengo haya marefu katika visiwa vya Zanzibar. Majengo haya yalitengenezwa viwandani Ujerumani na kusafirishwa hadi Zanzibar ambapo hapo yalisimamishwa tu. Yangali yapo na yanajulikana kama majumba ya 'Michenzani'.
Wasumbiji wangoja malipo ya kazi baada ya miaka 25
Takriban wafanyakazi 15,000 raia wa Msumbiji walifanya kazi za mikataba Ujerumani ya Mashariki katika miaka ya 1980. Wengi walirudi nyumbani baada ya kuungana Ujerumani ya Mashariki pamoja na Ujerumani Magharibi Oktoba 3, 1990. Serikali ya Msumbiji kamwe haikuwalipa mishahara yao kwa kazi waliyoifanya Ujerumani ya Mashariki. Wanaandamana mara kwa mara mjini Maputo mpaka leo.