Uholanzi mabingwa wa Ulaya
7 Agosti 2017Ni nguvu kubwa ya mchezo huo sasa inayozidi kukua katika bara hilo, kwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi pamoja na kupata idadi kubwa ya watu waliokuwa wakiangalia katika televisheni.
Idadi iliyoongezeka ya timu zilizoshiriki kufikia 16 kutoka 12 za hapo awali ilipandisha uhudhuriaji kufikia hadi watu 240,000 katika michezo 31, ikiwa ni juu kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopita ambapo waliohudhuria walifikia 217,000, wakati ambapo michezo yote ya mabingwa wa mashindano hayo Uholanzi tikiti zake zote zikiwa ziliuzwa.
Uholanzi iliishinda Denmark kwa mabao 4-2 na kocha wa Uholanzi alisema Denmark pia walicheza kandanda safi ya ushindani.
"Kulikuwa na timu mbili ambazo zilitaka kucheza kandanda, kucheza mchezo wa kumiliki mpira na kutaka hasa kushinda , licha ya kwamba ni ukweli usiofichika katika fainali , lakini mchezo ulioshuhudia mabao sita, tulikuwa bora hata hivyo, lakini Denmark pia walionesha kwamba wana uwezo mkubwa katika fainali, Nadim , Harder , na wengine wote waliweka mbinyo mkubwa, kwa hiyo nafikiri kwa mashabiki ilikuwa jioni nzuri na kwa upande wetu pia."
Viviane Miedema alifunga mabao mawili wakati wenyeji Uholanzi wakiishinda Denmark kwa mabao 4-2 jana Jumapili na kuwa taifa la nne kushinda ubingwa wa kandanda la wanawake barani Ulaya tangu michezo hiyo kuanza mwaka 1984.
Mwandishi: Sekione Kitojo/dpae,afpe,rtre,ape
Mhariri: Mohammed Khelef