Uhispania yawasaka wahamiaji 48 waliozama Canary
30 Septemba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa, mpaka sasa watu tisa wamethibitishwa kuwa wamekufa.
Ajali hiyo ilitokea wakati waokoaji hao walipokuwa wanajaribu kukikaribia chombo hicho.
Maafisa wa Uhispania wamesema matumaini ya kuwaokoa waliokuwamo ndani ya boti hiyo yamezidi kuwa finyu lakini wameeleza kuwa juhudi zinaendelea.
Soma zaidi: Watu 9 wamefariki baada ya boti yao kuzama karibu na Canary
Chombo hicho cha baharini kilichokuwa kinawasafirisha wahamiaji kilizama tangu Ijumaa usiku na miongoni mwa watu tisa waliokufa ni mtoto mmoja.
Waokoaji waliweza kuwaokoa wahamiaji 27.
Mamlaka ya Uhispania imesema wahamiaji hao wametoka Mali, Mauritania na Senegal.