1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania kutawala soka kwa miaka ijayo

2 Julai 2012

Uhispania iliingia katika kinyang'anyiro cha UEFA EURO 2012 kama timu bora ulimwenguni. Wiki tatu baadaye imeshinda kombe hilo na kudhihirisha hilo.

https://p.dw.com/p/15Q3A
KIEV, UKRAINE - JULY 01: Iker Casillas (C) of Spain lifts the trophy as he celebrates following victory in the UEFA EURO 2012 final match between Spain and Italy at the Olympic Stadium on July 1, 2012 in Kiev, Ukraine. (Photo by Laurence Griffiths/Getty Images)
UEFA EURO 2012 Spanien vs. Italien SiegPicha: Getty Images

Hakuna timu katika historia iliyowahi kushinda mataji matatu yakiwemo mawili ya ubingwa wa barani na moja la Ulimwengu mfululizo, na hakuna aliyewahi kuhifadhi taji la Ulaya.

Fauka na hayo, wahakiki katika dimba la UEFA EURO 2012 walikuwa wakiwataja mabingwa hao watetezi kuwa wa kuchosha. Utabiri kuwa timu zilizo na mbinu za wazi za soka kama vile Ujerumani, na kisha Italy zikafuata. Wote walikosea.

Kabumbu safi ya kusalia na mpira miguuni na kupiga pasi za uhakika na kisha kufanya mashambulizi kwa kasi iliiongoza Uhispania kwa ushindi wa magoli manne kwa sifuri dhidi ya Italy Jumapili katika uwanja wa Olimpiki mjini Kiev. Huku wakisaidiwa na mpinzani wao kupunguzwa hadi wachezaji 10 kufuatia jeraha katika dakika ya 64, Wahispania walikuwa moto w akuotea mbali na wakawanyisha kazi ngumu Italy.

Andres Iniesta ni nguzo muhimu katika ufanisi wa Uhispania
Andres Iniesta ni nguzo muhimu katika ufanisi wa UhispaniaPicha: Getty Images

Uhispania ilianza na ikamaliza dimba la UEFA EURO 2012 kwa kucheza dhidi ya Italy ijapokuwa sare ya goli moja kwa moja ya tarehe 10 Juni hakikuwa kitu chochote ikilinganishwa na mchezo wa jana Jumapili uliojaa mabao. Wachezaji wa Uhispania Cesc Fabregas, Xavi Hernandez, Andres Iniesta na nahodha Iker Casillas ni miongoni mwa wachezaji waliong'ara zaidi katika dimba hilo. Mchezaji bora wa Italy Andrea Pirlo pia anastahili kuwa katika orodha hiyo.

Mario Balotelli alikuwa bila shaka mchezaji aliyeonyesha umahiri zaidi kibinafsi katika dimba hilo kutokana na magoli yake mawili maridadi ya nusu fainali ambapo Italy iliwalaza Wajerumani magoli mawili kwa moja.

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini amesema alikuwa na wasiwasi mkubwa kabla ya kuanza kwa dimba la UEFA EURO 2012 lakini kinyang'anyiro hicho kimekuwa cha kufana ndani na nje ya uwanja, na kitawacha sifa kubwa katika soka ya Ulaya. Platini aliunga mkono ombi la Poland na Ukriane kuandaa tamasha hilo wakati nchi hizo mbili zilipochaguliwa mwezi Aprili mwaka 2007 muda mfupi baada ya kuwa rais wa UEFA.

Lakini kabla ya dimba hilo, kulikuwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ongezeko la gharama, kucheleweshwa dimba hilo katika nchi zote mbili, na hali tete ya kisiasa nchini Ukraine.

Wenyeji Poland na Ukraine wapongezwa kwa ufanisi
Wenyeji Poland na Ukraine wapongezwa kwa ufanisiPicha: picture-alliance/dpa

Alitishia mara kadhaa kuhamisha dimba hilo kutoka Ukraine. Lakini akizungumza kabla ya fainali, Platini alizisifu nchi zote mbili kwa kufanikisha fainali hizo.

Zaidi ya watu milioni 1.3 walihuhuria mechi hizo uwanjani, idadi ambayo imevunja rekodi. Alisema utazamaji wa mashabiki kupitia televisheni kote ulimwenguni siyo tu Ulaya, ulikuwa juu hata katika nchi ambazo hazikushiriki dimba hilo.

Platini vile vile alisifu soka iliyochezwa viwanjani akisema kulikuwa na ubora wa hali ya juu, pamoja na mbinu za kiufundi. Kwamba kulikuwa na usiamamizi mzuri wa waamuzi wa mechi ambao walifanya kazi yao kwa njia ya wazi na huru.

Mwandishi: Bruce Amani/reuters/dpa/afp
Mhariri: Mohammed Khelef