1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhariri:Soko la ajira linaigawa jamii

1 Mei 2013

Ujerumani imenusurika na mgogoro wa kiuchumi hadi sasa-na hilo linalihusu pia soko la ajira.Hata hivyo jamii imegawika nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/18Q3y
Prof. Dr. Christoph Köhler,mkurugenzi wa taasisi ya elimu jamii katika chuo kikuu cha Friedrich-Schiller huko JenaPicha: Köhler

Jamii nchini Ujerumani imegawika mara dufu:Kwanza kati ya watu wenye mapato ya juu na wale wenye mapato haba (au hata madeni)-na mwanya hapo umezidi kupanuka.Mgawanyiko wa pili unakutikana katika soko la ajira kati ya tabaka ya "kwanza" na tabaka ya pili.Hii ya pili ni ile ambayo wafanyakazi hulipwa mishahara duni,mikataba yao ya kazi si madhubuti au hawana kazi kabisa.Tabaka hii ya pili imezidi kukuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Nnatarajia, hali katika tabaka ya kwanza ya soko la ajira itaimarika kutokana na hali mpya katika medani ya idadi ya wakaazi nchini Ujerumani.Tunajikuta katika awamu ya kustaafu idadi kubwa ya watu waliozaliwa katika ule wakati ambapo uzazi ulikuwa mkubwa na kuingia katika awamu ya uhaba wa kizazi kipya..Kama inavyobainika, hali ni tulivu nchini Ujerumani licha ya migogoro katika eneo la kusini mwa ulaya na uchumi wa Ujerumani pia una nafasi nzuri katika masoko ya dunia.Kutokana na sababu hizo nafasi katika soko la ajira ni nzuri pia kwa watu waliosoma.Hofu walizonazo vijana wengi kuhusu maisha ya siku za mbele hazina msingi kwa hivyo.

Asili mia 15 wanaishi katika hali ya umaskini

Kuhusu tabaka ya pili katika soko la ajira,nnahisi mie hali si ya kutia moyo.Sekta ya kazi za mishahara duni imeanzishwa kati kati ya miaka ya 90.Kuimarika hali ya mambo katika soko la ajira ni ushahidi kwamba sekta hiyo tangu mwaka 2007 imefkia kiwango cha juu na wakati huo huo idadi ya wasiokuwa na kazi imepungua..Hiyo lakini sio sababu ya watu kushusha pumzi kwasababu tabaka ya watu wanaofanya kazi za mishahara duni wakichanganywa na idadi ya watu milioni tatu wasiokuwa na kazi inafikia jumla ya watu milioni 11.Idadi ya watu wanaoishi katika hali ya umaskini tangu mwaka 2007 imesalia kuwa asili mia 15.

Tabaka ya wafanyakazi wengi kama hao ni sumu sio tu kwa wahusika bali pia kwa jamii kwa jumla.Hali ya ukosefu ajira na kazi za mishahara duni ndio chanzo cha kuibuka tabaka nyengine ya jamii ambayo haina nafasi nzuri ya kubadilisha hali yao ya maisha.Hapo zinachanganyika hatari tangu za kiafya mpaka za kijamii zinazotokana na pato duni na umaskini wa uzeeni-hali ambayo inaweza baadae kuwaathiri pia watoto.Hoja kwamba watu wenye asili ya kigeni ndio wanaokumbwa na hali hiyo ni potofu kwasababu sehemu kubwa ya watu waliotumbnukia katika hali hiyo wana asili ya Ujerumani magharibi.

Mwandishi:Köhler,Christoph/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman