1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhaba wa mvua kuikumba Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika

25 Agosti 2022

Utabiri mpya uliotolewa Alhamisi kuhusu mvua za msimu wa mwezi Oktoba na Desemba katika kanda ya Mashariki na Pembe ya Afrika unaonesha kutakuwa na uhaba mkubwa wa mvua hizo za mwisho wa mwaka zinazotegemewa kwa uzalishaji wa chakula.

https://p.dw.com/p/4G37A

Utabiri huo uliochapishwa na kituo cha ufuatiliaji mwenendo wa hali ya hewa cha jumuiya ya mataifa ya Pembe ya Afrika IGAD, ICPAC, unasema nchi za Kenya, Ethiopia, Somalia na maeneo kadhaa ya Uganda na Tanzania ndiyo yatashuhudia hali mbaya. Kutaka kufahamu zaidi kilichobainishwa na hali itakuwa mbaya kwa kaisi gani, Rashid Chilumba amezungumza na Collison Lore afisa mwandamizi kwenye kituo cha ICPAC.