Ugiriki yaokolewa
21 Februari 2012Kupitishwa kwa mpango huo ndilo sharti la kukubali kwa wadai binafsi, ikiwa pamoja na mabenki na mashirika ya bima, kusamehe sehemu ya madeni yao. Makubaliano hayo yataiwezesha Ugiriki kulipunguza deni lake kwa asilimia 120.5 ya pato jumla la ndani hadi kufikia mwaka wa 2020 .
Katika muda wote wa mazungumzo mjini Brussels Waziri Mkuu wa Ugiriki Lucas Papademos alikuwa kiunganishi wa mawasiliano kati ya mawaziri wa fedha na wawakilisi wa wadai binafsi.
Kupitishwa mpango huo wa pili maana yake ni kwamba serikali ya Ugiriki itaendelea kuzitekeleza hatua za kubana matumizi ,ikiwa pamoja na kupandisha kodi kwa kiwango kikubwa na kuwapunguza watumishi wa serikali. Lakini hatua hizo zinapingwa vikali na wananchi.
Waziri wa fedha wa Ugiriki Evangelos Venizelos amesema kupitishwa mpango huo wa pili kutaondoa wasiwasi juu ya mustakabal wa Ugiriki
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Christine Lagarde amesema leo inaanza siku ambapo kiwango cha deni la Ugiriki kitakuwa asilimia 120.5 ya pato lake jumla la ndani. Hatua kubwa imepigwa haraka itakayoiweka Ugiriki katika hali nzuri zaidi ya kuutekeleza mpango wake kamambe ambao imekuwa inaufanyia mazungumzo kwa wiki kadhaa zilizopita.