Ugiriki yaifunga Urusi 1-0
18 Juni 2012Matokeo hayo yameifanya Urusi ifunge virago kuelekea nyumbani baada ya mahasimu wao katika kundi A Jamhuri ya Czeck kuinyuka Poland 1-0. Ushindi huo unaifanya Czeck kukaa kileleni mwa kundi A ikiwa na pointi sita na kuiacha Poland ambayo ni mwenyeji mwenza katika michuano hiyo kutupwa nje ya michuano wa UEFA 2012.
Kwa upande wa Ugiriki mashabiki wa soka wa taifa hilo watakwenda katika vituo vya kupiga kura leo hii katika awamu nyingine ya uchaguzi mkuu wa taifa hilo huku wakiwa na nyuso za furaha.
Nahodha wa timu hiyo Giorgos Karagounis, ambae aliipatia timu yake goli pekee la ushindi muda mfupi kabla ya kipindi cha pili alishangilia kwa kusema matatizo ya taifa lake yamekuwa kama changamoto ya ushindi huo.
Alijigamba kwamba wao wana uwezo lakini kwa namna nyingine matatizo waliyonayo yamechochea ushindi huo. Kama Ujerumani itashinda katika mechi yake ya leo dhidi ya Denmark itatoa fursa ya timu hiyo kukwaana na Ugiriki. Hapo kwa lugha iliyosikia kwe muda mrefu ni mpambano katika ya nchi iliyodidimia zaidi kiuchumi na mkopeshaji wake mkubwa Ujerumani.
Ama katika mchuno mwingine kati ya Jamhuri ya Czech na Poland, mchezaji wa kiungo Petr Jiracek aliinua mashabiki wa timu yake pale alitundika kimyani bao pekee la ushindi, pasipo uwepo wa nahodha timu hiyo Tomas Rosicky ambae alijeruhiwa.
Na jioni ya leo kutafanyika michezo ya kundi B ambapo Ujerumani itapambana na Denmark na Uhalanzi inahitaji Ushindi dhidi ya Ureno ili kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Mwandishi: Sudi Mnette/APE
Mhariri: Sekione Kitojo