1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yasema inaweza kutuma kikosi chote kinachohitajika Somalia

5 Oktoba 2010

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akihimiza juhudi za haraka zichukuliwe kuimarisha usalama ndani ya Somalia

https://p.dw.com/p/PVpY
Rais Yoweri Museveni wa UgandaPicha: AP

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa nchi yake pekee iko tayari kuongeza kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia-AMISOM na kufikia wanajeshi 20,000 ili kupambana na waasi wa Kiislamu wa Somalia. Matamshi hayo aliyatoa jana (04.10.2010) mjini Entebbe wakati akizungumza na Kamati ya Usalama ya mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Grace Kabogo alizungumza na msemaji wa Jeshi la Uganda, Luteni Kanali Felix Kulaije na kwanza anaelezea nia hiyo ya Uganda na jinsi suala hilo litakavyoshughulikiwa.

Mtayarishaji: Grace Patricia Kabogo

Mhariri:Josephat Charo