1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yaondoa mashtaka ya uhaini dhidi ya Kizza Besigye

Lubega Emmanuel11 Oktoba 2021

Hatua ya serikali ya Uganda kumwondolea mashtaka ya uhaini mkosoaji wake mkuu na kiongozi wa chama cha FDC, Dr. Kizza Besigye imepokelewa kwa maoni mseto.

https://p.dw.com/p/41XTt
Uganda Kizza Bezigye Opposition
Picha: DW/E. Lubega

Mwaka 2016 mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa, rais Yoweri Museveni alitajwa kuwa mshindi. Lakini upinzani ukiongozwa na Dr. Kizza Besigye na chama chake cha FDC walipinga matokeo hayo wakisisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda na kwa hiyo alikuwa tayari kuunda serikali mpya. Kanda ya video ilisambazwa ikionyesha  Dr. Besigye akiapishwa

Hatua hii ya kujitangaza mshindi, ilimfanya kiongozi huyo wa upinzani kukamatwa na kupelekwa kaskazini Mashariki mwa nchi ambako alifunguliwa mashtaka ya uhaini. Kesi dhidi yake iliendeshwa mfululizo kwa muda wa wiki kadhaa huku wafuasi wake wakitaka aachiwe.

Soma pia:Museveni atofautiana na mahakama kuhusu dhamana kwa wafungwa 

Kesi ya kisiasa dhidi ya wakosoaji

Ugandan opposition leaders Robert Kyagulanyi and Kizza Besigye
Picha: AFP/Getty Images

Kulingana na upande wa mashtaka palikuwa na ushahidi wa kutosha na kuridhisha kuwa mwanasiasa huyo alitenda makosa ya uhaini. Hata hivyo habari za mashtaka dhidi yake kuondolewa zimepokelewa kwa maoni mbalimbali. Uthman Katende, ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

Wengine wana mtazamo kuwa mashtaka ya uhaini hufunguliwa tu dhidi ya wapinzani kwa lengo la kudhibiti joto la kisiasa na mara nyingi hutupiliwa mbali kwa madai kuwa hakuna ushahidi.

Soma pia:Uganda yathibitisha kukamatwa kwa Lawrence Muganga

Vuguvugu jipya la siasa

Wakati huo huo hatua ya Dr. Besigye kuzindua vuguvugu jipya la kadi nyekundu wiki iliyopita wakidai kuanzisha harakati za kumng'oa Museveni madarakani imehusishwa na kuondolewa kwa mashtaka hayo na kwamba serikali inatuma ujumbe kuwa haibabaishwi na vuguvugu hilo la upinzani.

Dr. Kizza Besigye amenukuliwa akisema kuwa hata yeye mwenyewe hakujua kwamba mashitaka dhidi yake yameondolewa hadi pale aliposoma gazeti moja la humu nchini.