Uganda yakanusha madai ya kulisaidia kundi la M23
10 Julai 2024Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imetaja kuwepo uungaji mkono wa idara za ujasusi za Uganda kwa kundi la M23. Alipoulizwa na waandishi hbaari mjini Kampala, Naibu Msemaji wa masuala ya ulinzi wa taifa Deo Akiiki amepuuza tuhuma hizo akizitaja kuwa "kichekesho, zisizo na msingi wala haziingii akilini".
Amesema vikosi vya Uganda vimekuwa vikifanya kazi bega kwa bega na wenzao wa Kongo kusaidia kurejesha utulivu mwashariki mwa Kongo. Akiiki amebainisha kuwa nchi hizo mbili zinashirikiana kutengeneza mazingira ya kuwepo amani jambo ambalo limesaidia kuimarisha mahusiano yao.
Mbali ya Uganda, ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa pia imeitaja Rwanda kuwa na dhima kubwa kwenye mzozo wa Kongo kuwasaidia waasi wa M23.