Uganda: Mkutano wa Kimataifa kutoka kanda ya maziwa makuu wafanyika Kampala
6 Agosti 2012Matangazo
Mkutano huo utajadili kwa kina mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na namna ya kupata suluhu juu ya mzozo huo, ikiwemo kuundwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani na kupambana na waasi wa M23 wanaoyumbisha amani ya DRC.
Mkutano huo unajumuisha nchi 11, zikiwemo Angola, Burundi, Congo, Kenya, Rwanda, Sudan,Tanzania, Zambia na mwenyeji, Uganda.
Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo anahudhuria mkutano huo na Amina Abubakar amezungumza naye na mwanzo anatupa hali halisi ya mambo katika mji huo.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Othman Miraji