1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda kuilipa DRC zaidi ya dola bilioni 11?

9 Februari 2022

Mahakama ya Haki ya Kimataifa ICJ leo hii itatoa uamuzi wa endapo Uganda itapaswa kulipa kiasi cha zaidi ya dola bilioni 11 kama fidia kutokana na namna ilivyojihusisha katika mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,

https://p.dw.com/p/46jUp
DR Kongo | Nord Ost Ituri | Menschenrechtsverletzungen
Picha: Tom Peyre-Costa/NRC

Fidia hiyo inahusishwa na tuhumza za uovu zilizofanywa katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini la Ituri.

ICJ ni mahakama ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa, ambayo inajihusisha na utatatuzi  wa migogoro baina ya mataifa. Uamuzi wa kesi ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utatajwa katika kipindi kifupi kijacho. Mgogoro huo wa muda mrefu uliwasilishwa mahakamani hapo kwa mawa ya kwanza 1999.

DR Kongo | Nord Ost Ituri | Menschenrechtsverletzungen
Maeneo ya jimbo la Ituri DRCPicha: Tom Peyre-Costa/NRC

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa muda mrefu  2005 ICJ ilitoa uamuzi ambao ulionesha wazi kwamba Uganda ilikiuka sheria ya kimataifa kwa kuikalia sehemu ya mashariki jimbo la Congo kwa majeshi yake na kuyaunga mkono makundi yenye kujihami kwa silaha, katika kipindi cha vita ambacho kimedumu kuanzia mwaka 1998 hadi 2003.

Mataifa jirani kushindwa kufikia makubaliano ya usuluhishi.

Awali mataifa ya Afrika ambayo jirani na Congo yaliamrishwa kufanya majadiliano kuhusi fidia lakini 2015 irejea tena katika kizimba cha mahakama, ikisema hakuna hatua zilizopigwa katika mazungumzo hayo. Pande hizo kwa sasa zinasubiri uamuzi wa mwisho wenye kuhusu kiwango kikubwa cha fedha za malipo ya fidia.

Katika kikao cha kesi cha Mwezi Aprili, Uganda ilisema kiwangi kikubwa cha fedha kilichotajwa na Uganda kitavuruga uchumi wa taifa hilo na vilevile Congo hajitaoa ushahidi wa kutosha ya kuonesha kiwango cha hasara kilichopata wakati ule wa machafuko.

Lakini Congo kwa upande wake si kwamba inahitaji tu fidia kwa ajili ya wahanga wa Uganda kujihusisha katika mgogoro huo lakini pia uharibifu wa kiuchumi, athari kwa maliasili na wanyamapori.

Chanzo RTR