Uganda imetoa malipo ya kwanza ya fidia kwa Congo
12 Septemba 2022Uganda imetoa dola milioni 65 kama malipo ya kwanza ya dola milioni 325 iliyoamuriwa kulipa na Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ, kama fidia kutokana na taifa hilo kujihusisha katika mgogoro kwenye jimbo la Ituri mwishoni mwa miaka ya 1990.
Msemaji wa wizara ya fedha nchini Uganda Apollo Munghinda, amekiri fedha hizo kulipwa kwa jirani yake Kongo tangu Septemba mosi huku msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya akithibitisha kulipwa malipo hayo ya kwanza yanayotarajiwa kutolewa na Uganda katika awamu tano.
Katika kesi iliyoanzishwa dhidi ya Uganda mwaka 1999 Congo iliitaka mahakama ya ICJ kuiamuru Uganda kulipa bilioni 11 kama fidia kutokana na vifo, uharibu wa mali na uchumi uliosababishwa na jeshi la Uganda kuzingira baadahi ya maneno ya Congo miaka ya 90.