Ufunguzi wa kombe la dunia Urusi
14 Juni 2018Wahariri wameandika juu ya ufunguzi wa kombe la dunia nchini Urusi leo 14.06.2018 na mgogoro wa kuhusu sera ya wakimbizi Ujerumani
Gazeti la Badische Neuerste Nachrichten
Muda mfupi ujao ulimwengu utakodolea macho mjini Moscow. Na pengine michuano hii ya kombe la dunia mwaka huu heunda ikajenga daraja la kuifungulia upya milango nchi hiyo ya Urusi kuondokana na kutengwa kisiasa na kuzuia mchakato wa kuitenga kabisa nchi hiyo ambayo tayari kuporoka uhusiano wake na nchi za Magharibi kumeshaisbabishia hasara nchi hiyo. Hapa zaidi ni kuhusu jinsi ya kuishawishi tena Urusi kuwa mshirika. Na pangine hata kuwa jirani mzuri na rafiki.
Gazeti la Stuttgärter Nachriten
Tamasha hili la soka wanasema wanasoshologia kwamba ni tukio kubwa la kijamii linalowakutanisha watu katika wakati huu tulionao. Ronaldo anatazama,Messi anashangilia Pogba anashangaa huku akiwatakia kila la kheri Iceland. Kila mmoja wakati huu atakuwa kwenye msisimko ama wa kushangilia ushindi au majonzi ya kushindwa, na kilichowazi ni kwamba soka inaleta mshikamano japo wa muda mfupi,. Ni wapi kwingine kunakoweza kupatikana mkusanyiko wa dunia nzima?Ni kwenye mpira na pengine ndio sababu mpira ni duara japo unachezwa kwa dakika tisini na kumalizika kwake pia kunaleta majonzi.
Hamburger Abendblatt
Ujerumani imechukua tena nafasi. Mgogoro kuhusu wakimbizi umeligawa taifa hili na kuleta mpasuko Umoja wa Ulaya. Ni suala gumu na hasa inapohusu sera mpya. Kansela Merkel kwa muda mrefu ameonesha taratibu kujirekebisha kutokana na uamuzi wake wa mwanzo wa sera ya mlango wazi ambalo ilikuwa kosa lakini bila shaka hayuko tayari kukiri kosa hili.Hiyo itakuwa na maana ya kuridhia wahamiaji warudishwe mpakani wanapotaka kuingia kuomba hifadhi,na vile vile kuirudia sheria ya Dublin.Na bila shaka hiyo ni hatua itakayotowa ujumbe wa wazi kwa wahamiaji kwamba Ujerumani haiwezi kuwa nchi wanayoweza kukimbilia kujitafutia maisha bora.
Gazeti la Sächsische Zeitung
Kabla ya uchaguzi mkuu Hörst Seehofer alionesha kuna masikizano na amani kati yake na Kansela Merkel. Mtazamo wa Kansela Merkel wa kuikataa sera mpya ya wakimbizi Seehofer hakubaliani nao. Ni kitu cha kushangaza kiasi kwamba idadi ya wakimbizi sasa imeonekana kupungua sana. Lakini badala yake mgogoro huu wa wakimbizi unaweza kuiporomosha serikali.
Gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung
Wengi wanatikisa kichwa wakimtazama Kansela Angela Merkel.Inakwendakwendaje kutaka kumpiga breki waziri wake wa mambo ya ndani?Haswa pale ambapo anaonesha kuwa na mpango barabara wa sera mpya kuhusu wakimbizi. Ila hilo Kansela Merkel hakubaliani kabisa na mpango wa kuwarudisha wakimbizi wanapofika mpakani kwa Ujerumani.Kwa upande mwingine anapinga suala hili kuangaliwa kitaifa,anataka sheria mpya zijadiliwe kikanda miezi kadhaa ijayo.
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman