Ufaransa imemkamata aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Roger Lumbala, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu. Lumbala ni mbunge wa zamani aliyeongoza chama cha RCD-N, kinachodaiwa kutekeleza mauaji ya kiholela wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo kati ya mwaka 1998-2003. DW imezungumza na mwandishi Saleh Mwanamilongo kuhusu hatua hiyo.