1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaadhimisha Siku ya Taifa chini ya ulinzi mkali

14 Julai 2023

Ufaransa inaadhimisha leo Siku ya Taifa, maarufu kama Siku ya Bastille ambayo inafanyika chini ya ulinzi mkali ikiwa ni wiki mbili tu baada ya maandamano yenye vurugu kuitikisa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4TtiE
Frankreich Paris | PM Modi bei Feierlichkeiten zum Tag der Bastille
Picha: Aurelien Morissard/AP/picture alliance

Karibu maafisa wa polisi 45,000 watashika doria kote nchini leo jioni. Serikali inalenga kuzuia marudio ya machafuko yaliyoshuhudiwa mwishoni mwa Juni, kufuatia tukio ambalo polisi alimuuwa kijana mmoja.

Sherehe za kila mwaka za Siku ya Taifa, ambazo zinaadhimisha kuvamiwa kwa gereza la Bastille mwanzoni mwa Mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka wa 1789, huanza kwa maonyesho ya guaride la kijeshi asubuhi ambapo watu 5,000 walifurika katika mtaa wa Champs Elysees.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ndiye mgeni maalum wa maadhimisho ya mwaka huu. Mapema leo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimtunuku Modi tuzo ya heshima ya juu kabisa inayotolewa na rais nchini humo.

Ofisi ya Rais imesema tuzo hiyo ya Legion of Honour inaonyesha jukumu ambalo Modi amefanya katka kuweka mahusiano bora ya urafiki kati ya Ufaransa na India.