1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa na Uingereza zakubaliana kukabiliana na uhamiaji

20 Agosti 2015

Uingereza na Ufaransa zimetangaza kuzinduliwa kwa kituo kipya cha kuthibiti ulanguzi wa wahamiaji huku bara la Ulaya likikabiliwa na tatizo kubwa zaidi la wahamiaji tangu vita kuu vya pili vya dunia

https://p.dw.com/p/1GJ6A
Frankreich Bernard Cazeneuve und Theresa May in Calais
Picha: Reuters/R. Duvignau

Chini ya makubaliano ambayo yametiwa sahihi kati ya waziri wa maswala ya ndani wa Uingereza na mwenzake wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, Kundi kutoka Uingereza litasaidia kusambaratisha magenge ya kulangua binadamu na kupunguza juhudi za kisiri kuwavusha na kuwaingiza nchini Uingereza.

Uingereza na Ufaransa zimetangaza mbinu mpya za kiusalama kukabilina na walanguzi wa binadamu na kiasi cha euro milioni 10 zitatolewa na serikali ya Uingereza kusaidia wanaotafuta hifadhi na pia kuwarejesha wengine nyumbani. Maafisa wa polisi wa Uingereza watashika doria huko Calais kukabiliana na magenge yanayolangua wahamiaji na wakimbizi kupitia kivukio hicho.

Bandari hiyo ya kaskazni mwa Ufaransa imehanikiza vyombo vya habari vya Uingereza msimu huu wa kiangazi huku wakimbizi wakifanya juhudi za kufa na kupona kuingia kupitia njia hiyo ya chini na kuingia Uingereza na hata wengine wakipoteza maisha yao.

Flüchtlinge in Calais
Mazingira wanamoishi wahamiaji katika mji wa CalaisPicha: DW/H. Tiruneh

Wakiongozwa na kamanda mmoja Muingereza na mwingine Mfaransa wa ngazi za juu, maafisa hao watafanya kazi katika kituo hicho cha uthibiti kitakachojengwa karibu na kivuko cha kuingia Uingereza.

Makubaliano hayo yanajumuisha vikosi vya polisi vya Ufaransa, utafutaji wa ziada kwa kutumia meli, na kufanya kituo cha reli huko Calais kuwa salama kwa kuweka uwa, kamera za CCTV na kuwepo kwa teknolojia ya kutaadharisha dhidi ya mafuriko.Pia itaimarisha usaidizi wa kibinadamu kwa wahamiaji ili kukabiliana na hali mbaya ya mazingira wanamoishi ya Calais.

Watu 3000 kutoka Afrika, Mashariki ya kati na Asia wamepiga kambi huko Calais wakijaribu kuelekea Uingeraza ambapo wengi wana familia zao na kutafuta kazi wanaoiona kupatikana kwa urahisi. Watu Kumi wanahofiwa kufariki tangu mwezi Juni wakijaribu kuvuka.

Ufaransa na Uingereza wamejaribu kufanya juhudi za pamoja lakini l swala hili limeathiri uhusiano kati ya wanasiasa mjini London wakishutumu utepetevu wa vitengo vya usalama,huku Ufaransa ikilalamika kuwa ni rahisi kwa wahamiaji kufanya kazi bila idhini nchini Uingereza na hivyo kuwavutia katika pwani yake.

Keith Vaz ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayoisimamia wizara ya May, alikubali mkataba huo lakini akaonya kuwa kuna ushahidi tayari na mkubwa wa shughuli haramu katika vivukio vingine vya bandari za Ufaransa,Ubelgiji na Uholanzi.Amesema kuwa kufunga njia moja tu inamaanisha tatizo linahamia bandari nyingine.

Frankreich Flüchtlinge am Eurotunnel Calais
Wahamiaji wakivuka kuingia UingerezaPicha: Reuters/P. Rossignol

Alisema wanahitaji makubaliano kati ya mataifa ya pwani ya kaskazini haswa Ulaya kusitisha hali hii kabla hakujashuhudiwa mikasa mingine kama ilivyo Kalais ikifanyika katika bandari nyingine katika bara lote.

Uingereza imeahidi kutoa pauni milioni 22 sawa na Uro milioni 31 au dollamilion 34 kufikia sasa ili kuweka usalama katika Kivukio cha ufaransa.

Waziri mkuuu wa Uingereza David Cameron aliahidi kuzungusha uwa zaidi,kutoa rasilmali zaidi , na kikosi zaidi cha mbwa wa kunusa ili kuwasaidia maafisa wa polisi wa Ufaransa.

Uimarishaji usalama umesababisha bei wanaolipa wahamiaji na wakimbizi hao kwa magenge ya walanguzi kuongezeka kabla ya kuwavukisha.

Kulingana na mfanyikazi mmoja wa shirika lisilo la serikali,Usafiri wa lori uligharimu Uro 500 miezi michache iliyopita lakini sasa ni kati ya Uro 800 na 900 kwa sababu kuna maafisa wengi wa polisi na mbwa wa kunusa.

Shirika la hudumu cha Kivukio hicho Eurotunnel limesema kwamba juhudi za kuziba njia ya reli inayopitia chini imepunguza idadi hadi 150 kwa usiku mmoja wiki hii kutoka 1,700 mwishoni mwa mwezi July.Idadi hiyo ni pamoja na juhudi za wakimbizi hao hao.

Idadi ya wanaotaka kufika Uingereza ni ndogo ukilinganishwa na wanaoelekea mataifa mengine ya Uropa haswa Ujerumani ambayo ilisema wiki hii kuwa inatarajiwa wanaotafuta hifadhi kufikia elfu mia 8 badala ya elfu mia 5 ilivyo tarajiwa mwaka huu wa 2015 .Chansela wa Ujerumani Angela Merkel alionya siku ya Jumapili kuwa swala hilo huenda litakuwa changamoto kwa muungano wa Ulaya kuliko mzozo wa deni la Ugiriki

Nalo shirika la mipaka la Muuungano wa Ulaya liliripori kuwepo kwa wahamiaji elfu 107 na mia 5 katika mipaka ya muungano wa ulaya mwezi uliopita.

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya wahamiaji wanaowasili Ugiriki inayokabiliwa na mzozo inapanda huku karibu elfu 21 wakitua katika visiwa vya Ugiriki wiki iliyopita pekee.

Mwandishi: Bernard Maranga afp

Mhariri:Iddi Ssessanga