1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa inapiga vita ukeketaji

Suzanne Kraus / Maja Dreyer7 Desemba 2006

Mwaka 1979 kwa mara ya kwanza nchini Ufaranya kumeendeshwa kesi dhidi ya Mwafrika aliyehamia nchini humu na aliyekuwa baba wa msichana aliyefariki dunia baada ya kukeketwa. Tukio hilo liliishtusha jamii ya Kifaransa lilikuwa mwanzo wa juhudi nyingi dhidi ya ukeketaji.

https://p.dw.com/p/CHlz
Vifaa vinavyotumika kuwakeketa wasichana
Vifaa vinavyotumika kuwakeketa wasichanaPicha: africa-photo

Bado lakini wasichana wanakeketwa katika nchi hii. Kwa sababu hiyo, serikali ya Ufaransa, mwaka huu umeamua kuchukua hatua nyingine za kupiga vita desturi hiyo mbaya. Leo kunafanyika mkutano wa kwanza wa kuimarisha sera hiyo mpya.

Katika wimbo wake mpya, mwimbaji maarufu wa Ufaransa, Jeanne Cherhal, anaimba kuhusu maumivu wa msichana mmoja ambaye alikeketwa. Ni kitu kipya kabisa nchini humo kwa Mfaransa mzungu kuimbia suala hilo katika nyimbo zake, lakini anataka desturi hiyo mbaya ifutwe.

Pia ni lengo lake Nafissatou Fall. Tangu miaka 15 sasa mwanamke huyu wa kutoka Senegal anapiga vita dhidi ya ukeketaji mjini Le Havre ambapo wahamiaji wengi wa kutoka barani Afrika hukaa. Chini ya wenzake Wasenegal, Bibi Nafissatou Fall ni mtu anayetia aibu, lakini Nafissatou havunji moyo. Tena juhudi zake zinaleta faida, anasema bibi huyu: “Najua kwamba kila ninachofanya ni kitu kizuri. Hivyo tuliweza kuwaokoa wasichana wengi kutokeketwa. Zamani wasichana wote walikeketwa kabla hawajafika umri wa miaka minne. Lakini leo hakuna hata msichana mmoja anayeingia shule akiwa na umri wa miaka sita ambaye anakeketwa, kwa sababu hadi kufikia umri huu watoto wote nchini humu huchungzwa na madaktari. Hata hivyo, inabidi tuendelee kupiga vita ukeketaji."

Kwa mujibu wa Bibi Nafissatou, wazazi wanajua kwamba kuna sheria inayopiga marufuku ukeketaji. Kwa hivyo wanasubiri tu wasichana kufika umri ambapo hakuna hatari kukeketwa kwake kunaweza kugunduliwa na daktari. Wakizidi miaka 12 au 13 madaktari wa shule hawaruhusiwi tena kuwachungua wasichana kwenye mwili mzima. Huko sasa wazazi wanawapeleka wasichana nyumbani Afrika na kuwakeketa huko. Au kunafanyika kabla ya harusi yao.

Yale yanayotokea mjini Le Havre, yanatokea katika nchi mzima. Hasa ni wasichana kijana ambao ni wahanga wa desturi ya ukeketaji. Serikali ya Ufaransa inaongeza jitihada zake za kuwalinda wasichana hawa. Kutokana na sheria mpya inayopiga marufuku matumizi ya nguvu dhidi ya wasichana na wanawake, wasichana walikeketwa dhidi ya uamuzi wao wana haki ya kuwashtumu wazazi wake au wale wahusika hadi kufikia miaka 38. ´

Sasa pia wasichana wa asili ya kigeni wananufaika kutokana na sheria hiyo. Vile vile madaktari hawalazimiki tena kukaa kimya ikiwa wamegundua kesi ya ukeketaji wa wasichana. Na serikali ya Ufaransa inataka kuchukua hatua nyingine za kuwaelemisha jamii na kupiga vita ukeketaji.