Hali ya wasiwasi inatanda katika pembe ya Afrika kufuatia makubaliano ya kushtukiza kati ya Ethiopia na Somaliland. Somalia imelaani mpango huo ambapo Ethiopia inaitambua Somaliland kama nchi huru. Lakini kuna tofauti gani kati ya Somalia na Somaliland?