1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA EURO 2012: Uhispania fainali

28 Juni 2012

Uhispania imefanikiwa kutinga kwa mara ya tatu katika fainali ya mashindano makubwa duniani katika kipindi cha miaka sita,baada ya kuwashinda majirani zao Ureno kwa mikwaju ya kwa penalti 4-2 katika nusu fainali.

https://p.dw.com/p/15N0x
Spain's players celebrate after defeating Portugal after Euro 2012 semi-final soccer match at the Donbass Arena in Donetsk, June 27, 2012. REUTERS/Eddie Keogh (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER TPX IMAGES OF THE DAY)
Uhispania wakishangiria ushindi nusu fainali Euro 2012Picha: Reuters

Baada ya pambano hilo la vuta nikuvute kumalizika kwa sare ya bila kufungana hadi muda wa nyongeza , katika uwanja wa Donbass Arena, Cesc Fabregas aliweka mpira wavuni ikiwa ni mkwaju wa mwisho wa penalti hizo, na kuielekeza Uhispania katika fainali siku ya Jumapili, ambapo wanasubiri mshindi wa nusu fainali nyingine leo kati ya Ujerumani na Italia.

Xabi Alonzo na Joao Moutinho wote walikosa penalti zao wakiwa wa kwanza kutoka kila timu kujaribu bahati zao mbele ya walinda mlango wa timu hizo, lakini Ureno ilitanabahi mapema kuwa mambo yanaenda kombe baada ya mlinzi kutoka Zenit Saint-Petersburg ya Urusi Bruno Alves kuibamiza penalti yake katika mlingoti wa goli.

Portugal's Pepe wipes tears after the lost their Euro 2012 semi-final soccer match against Spain at the Donbass Arena in Donetsk, June 27, 2012. REUTERS/Alessandro Bianchi (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Mlinzi wa Ureno Pepe akisikitika kwa kutolewa mashindanoniPicha: Reuters

Uhispania yafurahi kufika fainali

"Tumefurahi sana kufikia fainali. Sijui iwapo kitu kama hicho kuwa hakijafanyika katika historia ", Fabregas ameiambia televisheni ya nchi yake, huku sauti yake ikisikika ikiwa na furaha kuu.

"Waliniambia nitapiga mkwaju wa pili katika penalti hizo, lakini nilisema, hapana, nataka kupiga ya tano ".Ameongeza Fabregas. Fabregas amekuwa na bahati ya kutoa mchango muhimu kwa timu yake ya taifa wakati unahitajika.

Penalti yake ya ushindi dhidi ya Ureno katika nusu fainali ya Euro 2012 jana Jumatano , imeongezea katika jumla ya mchango huo ambao ni pamoja na kutayarisha bao la ushindi katika fainali ya mwaka 2010 ya kombe la dunia. Italia ambayo huenda ikawa mpizani wa Uhispania katika fainali ya mwaka huu, pia inakumbuka penalti yake ya ushindi katika pambano lao la robo fainali katika kombe lililopita la kombe la Ulaya.

Mabingwa hao wa dunia na watetezi wa taji hili la Euro , Uhispania, wanajaribu kuwa timu ya kwanza katika historia kushinda mataji matatu mfululizo katika mashindano makubwa.

Mwisho wa kusikitisha kwa Ronaldo

Ni mwisho wa kukatisha tamaa kabisa katika mashindano haya kwa nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo, ambaye ametishia kuwa ataipeleka timu yake katika fainali yake ya pili ya mashindano makubwa katika historia , lakini hata hakupata nafasi ya kupiga mkwaju wake wa penalti.

Portugal's Cristiano Ronaldo reacts during the Euro 2012 semi-final soccer match against Spain at Donbass Arena in Donetsk, June 27, 2012. REUTERS/Charles Platiau (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Nyota wa Ureno Cristiano RonaldoPicha: Reuters

"Iwapo ningetakiwa kuchagua njia ya kushindwa, nisingechagua njia hii", amesema kocha wa Ureno Paulo Bento. Lakini ni lazima ushindwe wakati fulani, amesisitiza. Uhispania ni timu kubwa na tunaweza kutoka uwanjani vifua mbele.

Portugal's coach Paulo Bento reacts during their Euro 2012 semi-final soccer match against Spain at the Donbass Arena in Donetsk, June 27, 2012. REUTERS/Alessandro Bianchi (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Kocha wa Ureno Paulo BentoPicha: Reuters

Chaguo la kushangaza katika kikosi cha Uhispania , Alvaro Negredo alikuwa chanzo cha nafasi ya kwanza ya kupata bao katika mchezo huo, wakati Alvaro Arbeloa alipommegea pasi wakati mshambuliaji huyo wa Sevilla alipokuwa na kundi la walinzi wa Ureno katika eneo la hatari la timu hiyo.

Ronaldo ambaye alipachika mabao yote ya ushindi katika mchezo dhidi ya Uholanzi na jamhuri ya Czech, alikuwa mtazamaji tu katika dakika kumi za mwanzo, lakini taratibu ushawishi wake ulianza kujitokeza.

Baada ya kupiga vibaya mkwaju wa adhabu na kurudishwa na walinzi wa Uhispania , alipiga mpira mwingine juu ya goli akiwa karibu na eneo la hatari la Uhispania , na kisha kutandika mkwaju mwingine ambao ulitoka nje kidogo ya goli la Uhispania.

Kama katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Ufaransa, Uhispania ilipata taabu pia kupata matundu ya kupitisha mpira yao katika ukuta wa maadui.

Maelfu ya mashabiki wa Uhispania walikusanyika mjini Madrid kushuhudia pambano hilo dhidi ya Ureno, na kuamsha shamra shamra kubwa mara baada ya ushindi huo wa mabao 4-2.

Spain's Cesc Fabregas reacts after scoring the winning penalty goal against Portugal during the penalty shoot-out in their Euro 2012 semi-final soccer match at the Donbass Arena in Donetsk, June 27, 2012. REUTERS/Juan Medina (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER TPX IMAGES OF THE DAY)
Cesc Fabregas akishangilia bao lake la ushindi kwa UhispaniaPicha: Reuters

Hali ilikuwa ya shauku kubwa hata kabla ya kupigwa penalti hizo mjini Donetsk, nchini Ukraine, huku kukisikika sauti za miluzi na fashifashi katika mji huo mkuu wa Uhispania kabla hata penalti ya kwanza kupigwa.

Nani mbabe

Leo jioni (28.06.2012) ni zamu ya Ujerumani na Italia kuonyeshana kazi. Timu ya Ujerumani inawania kwa mara ya kwanza kuiangusha Italia katika mashindano makubwa. Wajerumani hawana imani kubwa ya ushindi dhidi ya Italia , lakini mchezaji wa kiungo Bastian Schweinsteiger, amesema ikiwa Ujerumani , imeweza kuishinda , Uholanzi, Uingereza, Ureno na Brazil, sasa ni zamu ya Italia. Kama hayo yatatokea ni suala la kusubiri na kuona.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre/ afpe