1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA-2012-Makadirio ya mechi za kundi B

13 Juni 2012

Homa ya dimba ikoje kabla ya michuano ya kundi B, kwanza kati ya Danemark na Ureno, na baadae kati ya mafahali wawili wa jadi, Ujerumani na Uholanzi.

https://p.dw.com/p/15DpT
Fan-Zone in Donezk, Ukraine (fussball, Euro-2012) Datum: 12.06.2012 (c) DW, Karina Oganesian zugeliefert von Dmytro Kaniewski
UEFA EURO 2012 -Mashabiki huko Donezk nchini UKrainePicha: DW/Oganesian

Tuanzie na alifu yaani pambano la hivi punde kati ya Danemark na Ureno huko Lemberg. Licha ya kuondolewa patupu moja bila na Ujerumani katika pambano la awali, wanasoka wa Ureno wanaamini bado wanaweza kusonga mbele katika michuano ya kombe la Ulaya Euro 2012. "Tukiranda kama tulivyoranda dhidi ya Ujerumani, basi tunaweza kushinda, anaashiria mshambuliaji wao anaeichezea timu ya Uingereza ya Manchester United, Nani.

Danemark, lakini, ambayo iliifunga Uholanzi moja kwa bila katika pambano lao la mwanzo la kundi B, haitopakata mikono ."Tunajua vipi kuwashinda wareno", anasema kocha wao, Morten Olsen, akakumbusha pambano la Oktoba mwaka jana ambapo Danemark iliifunga Ureno mabao mawili kwa moja. "Kumbukumbu zetu dhidi ya Ureno ni nzuri, tumecheza mara tano katika kipindi cha miaka mitano niliyopiota dhidi yao na tumeshinda mara mbili na kushindwa mara moja tu."Amesisitiza Morten Olsen.

Kwa ushindi wao wa moja kwa bila dhidi ya makamo bingwa wa dunia, Uholanzi, wadenmark wamefufua maajabu waliyoyazusha walipoondoka na taji mwaka 1992 baada ya kuwashinda kwanza Uholanzi na baadae mabingwa wa dunia kutoka Ujerumani na kuondoka hatimae na kombe la Ulaya.

UEFA EURO 2012 Europameisterschaft Portugal vs Dänemark Fans
UEFA EURO 2012 Mashabiki wa DanemarkPicha: AP

Ama kuhusiana na pambano la leo usiku, mafahali wawili wa jadi-Ujerumani na uholanzi- wamedhamiria kuweka kando uhasama wao katika uwanja wa dimba na kujishughulisha na kimoja tu: nani ataondoka na pointi tatu firimbi ya mwisho itakapolia.

"Kila mtu anajua Uholanzi inakabiliwa na kishsindo kikubwa," anasema kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Löw, akikumbusha jinsi Uholanzi ilivyoondolewa moja bila na Danemark hapo awali.Hata hivyo, wanasoka wa Ujerumani wanatambua haitakuwa kazi rahisi.

Mchezaji wa kati, Bastian Schweinsteiger, anasema anaamini litakuwa pambano kali kupita kiasi.

Hata hivyo, kocha Joachim Löw hakufichua bado kama anapanga au la kuubadilisha muundo wa timu yake iliyoteremka uwanjani dhidi ya Ureno.

Fußball Bundestrainer Joachim Löw Euro 2012 Kader
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim LöwPicha: picture-alliance/dpa

Makamo bingwa wa dunia wanaweza kuyapa kisogo mashindano ya fainali za kombe la Ulaya Euro 2012 pindi wakishindwa kufua dafu leo usiku dhidi ya Ujerumani na kama Danemark itaondoka angalao na pointi moja katika pambano lake dhidi ya Ureno.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters,SID

Mhariri.Miraji Othman