1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udhibiti mkali zaidi wa bajeti wahitajiwa Umoja wa Ulaya

13 Mei 2010

Halmashauri Kuu ya Ulaya,imewasilisha mapendekezo ya kuimarisha uratibu wa bajeti,kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/NMc6
European Commissioner for Economic Affairs Olli Rehn speaks during a media conference at an emergency meeting of EU finance ministers in Brussels, Sunday, May 9, 2010. EU finance ministers meet in Brussels Sunday to discuss establishing a new "stabilisation mechanism" to prevent the Greek debt crisis from spreading. (AP Photo/Virginia Mayo)
Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Fedha katika Umoja wa Ulaya,Olli Rehn.Picha: AP

Mkuu wa masuala ya uchumi na fedha katika Umoja wa Ulaya,Olli Rehn amesema, kuanzia mwaka 2011,miswada ya bajeti za nchi wanachama, iwasilishwe Brussels kabla ya kuidhinishwa na mabunge yake.

Sera za fedha katika Umoja wa Ulaya, lazima ziratibiwe hapo awali, ili bajeti ya nchi moja isijekuhatarisha uchumi wa wanachama wengine. Hata kanuni za miradi ya kuimarisha na kufufua uchumi,zinapaswa kuwa kali zaidi. Kwa njia hiyo, hali ya madeni ya serikali za kitaifa itaweza kudhibitiwa vizuri zaidi.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) gibt am Mittwoch (05.05.2010) eine Regierungserklärung zur Griechenland-Hilfe im Bundestag in Berlin. Deutschland beteiligt sich am internationalen Rettungspaket für Athen mit 22,4 Milliarden Euro Krediten in drei Jahren. Foto: Hannibal dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: picture alliance/dpa

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ameunga mkono pendekezo hilo la kutaka udhibiti mkali zaidi wa nakisi za bajeti katika Umoja wa Ulaya. Amesema, haamini kuwa hatua hizo kali zinaopunguza mamlaka ya mabunge ya kitaifa.Mfumo mkali wa kusimamia miradi ya kuleta utulivu na kufufua uchumi ni utaratibu ulio sahihi.

Mwandishi: P.Martin/ZPR