1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi wa bomoabomoa Zimbabwe

4 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CExN

Harare:

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa akiwa katika ujumbe muhimu wa kutathmini harakati za bomoa bomoa nchini Zimbabwe, Mtanzania Anna Tibaijuka, ataongeza muda wake wa kutembelea nchi hiyo kwa siku tano. Bibi Tibaijuka, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, Habitat, lenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya atakuwa nchini Zimbabwe hadi Ijumaa na kutathmini hali halisi ilivyo kutokana na zoezi hilo la bomoa bomoa ambalo limewafanya Wazimbabwe elfu kadhaa kutokuwa na makazi. Bibi Tibaijuka amewasili Harare Juni 26 kwa lengo la kutathmini athari za kibinaadamu zinazosababishwa na uvunjaji wa nyumba ambao Rais Robert Mugabe anasema kuwa una madhumuni ya kuifanya Zimbabwe isiwe na madongo poromoka na kupunguza ujambazi. Kwa mujibu wa makisio ya Umoja wa Mataifa watu wapatao Laki mbili wamevunjiwa nyumba zao wakati ambapo upinzani unasema kuwa ni watu millioni moja na nusu.