Uchumi wa Ujerumani ; Wenye viwanda watoa mtazamo.
30 Julai 2009Ikiwa bingwa wa uuzaji bidhaa nje ya nchi, Ujerumani inategemea sana hali ya uchumi wa dunia. Ndio sababu mzozo wa kifedha umeathiri mno uchumi wake na kusababisha Ujerumani kutoa kichocheo cha uchumi ili kupambana na mzozo huo wa kimataifa. Wataalamu wanasema uchumi wa Ujerumani utapungua kwa asilimia sita ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Lakini pamoja na hayo kuna matumaini kiasi. Hali ya kushuka inaanza kubadilika , na inaanza kupanda taratibu, wanasema wadadisi wa masuala ya kiuchumi.
Viwanda vya kemikali ni miongoni mwa sekta nne muhimu za viwanda nchini Ujerumani , kandoni mwa viwanda vya magari , mashine na vifaa vya umeme. Sekta hii inawafanyakazi wapatao 430,000, ikiwa hivi sasa hali si nzuri. Na uzalishaji katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imepungua kwa asilimia 15,5 na uuzaji nje umepungua kwa asilimia 12. Pamoja na hayo rais wa chama cha wenye viwanda vya kemikali , ambaye ni mkuu wa kiwanda cha Henkel Ulrich Lehner, anasema kuwa kuna matumaini katika hali ya tathmini ya viwanda hivyo.
Tukiangali huko mbele , pamoja na kuwa na wingu la kuporomoka kwa uchumi tunaweza kuona mwanga mbele ya upeo wa macho yetu. Katika miezi iliyopita uzalishaji umeongezeka. Hali hii inaeleza mengi , kwamba baada ya mporomoko huu mwishoni mwa mwaka jana katika sekta ya viwanda vya kemikali tumeweza kufika mwisho wa mporomoko.
Baada ya hapo tumekuwa na matumaini katika sekta nyingine, sekta ya makampuni ya vifaa vya electroniki ambayo nayo mapato yake yamepungua. Makampuni haya yanatambua kuwa ni kwa njia tu ya uhifadhi na sio ukuaji ndio yataweza kuendelea. Na hata mabenki pia yanachukua tahadhari, kama ilivyo kwa Deutsche bank. Kwa mapampuni yanayotengeneza madawa pia mapato yao yamepungua, lakini utawala wa makampuni hayo unaeleza matumaini yenye tahadhari. Na pia kiwanda cha magari cha Daimler imepoteza mabilioni ya Euro katika robo ya pili ya mwaka huu. Na pia soko la hisa limepoteza kuliko sekta nyingine. Kwa mujibu wa Chris-Oliver Schickentanz kutoka Commerzbank anasema kutokana na hali hiyo Daimler haiko peke yake.
Hili ni tukio baya katika ripoti nzima ya msimu. Tunakumbushwa kwa mara nyingine tena kwamba kuna hali inayoendelea ya mporomoko. Lakini inakuja katika hali ambayo si mbaya hivyo, kama tulivyofikiria. Hii ina maana matarajio yalikuwa madogo sana . Kwa mujibu wa hayo wadadisi wanaona kuna hali ya kupanda. Hii ina maana hali ya mporomoko inapungua. Na hii ndio ishara ya mwanzo, kuelekea katika mwelekeo sahihi, katika kuimarisha hali hii.
Hata kama uchumi utaanza kukua katika sekta mbali mbali katika soko la kazi mzozo bado haujazuiliwa. Hii inawezekana kuwa uchumi wa Ujerumani katika majira ya mapukutiko utakuwa bado katika matatizo.
Mwandishi Michael Braun/ ZR / Sekione Kitojo.
Mhariri Mohammed Abdulrahman.