Vigogo wadondoka
6 Agosti 2015Meli zilizopo baharini dunia nzima leo zitakuwa zikipiga honi, kuadhimisha kufungukiwa tena kwa Mfereji wa Suez uliopo nchini Misri.
Afisa Mkuu wa Mamlaka Mohab Mohamed Hussein Mameesh, amesema sasa chakula kitawasili kwa haraka zaidi. Madawa yatawasili haraka. Bidhaa za mafuta ya petroli zitawasili haraka. Aliongeza kuwa, Misri inaitumikia dunia nzima kwa kuupanua mfereji huwo.
Chakula chawasili
Mfereji huwo mpya uliojengwa pembezoni mwa ule wa zamani - utaruhusu meli kupishana, kama vile ilivyo katika barabara za gari, tofauti na ilivyokuwa zamani, meli moja tu ndio ikiweza kupita katika mfereji huo.
Wakati mfereji huo utakapokamilika, meli nyingi zaidi zitaweza kuusafiria kwa wakati mmoja, na hili litasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa baadhi ya meli kutoka muda wa masaa 22 ilivyokuwa zamani hadi masaa 11.
Mameesh amesema meli zinazoundwa siku hizi ni kubwa sana, uwezo wa mfereji huwo kwa sasa unaruhusu meli nane tu kuusafiria kwa siku. Kutakapokuwa na meli tisa, basi moja inalazimika kusubiri nje ya mfereji. Baada ya upanuzi, Mamlaka ya Mfereji huwo imesema hadi mwaka 2023 inatarajia kuingiza zaidi ya dola bilioni 13 za kimarekani kwa mwaka kutokana na malipo ya ushuru, au dola bilioni tano zaidi ya kipato kinachopatikana kwa sasa.
Walipa kodi walalamika
Hata hivyo wadadisi wanasema jitihada alizozichukuwa rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi kuupanua mfereji huwo, ni njia ya kuitafutia serikali yake uungwaji mkono zaidi huku nchi hiyo ikiwa na matatizo kadhaa ya kiuchumi.
Mtendaji Mkuu wa shirika la kikanda la ushauri wa kutabiri lilioko Cairo, Angus Blair, amesema kuna masuali kadhaa juu ya kustahili kwa mradi huo mzima. Misri bado ipo katika hali mbaya, ongezeko la watu linazidi kukua, ukuwaji wa kiuchumi unashuka, huku mfumuko wa bei ukibaki kuwa juu, halikadhalika wananchi sasa wameamka kisiasa.
Profesa wa historia ya somo la majini wa chuo cha King's College cha London amesema, hata mradi huwo ukifanikiwa hauwezi kutosheleza kuimarisha maisha ya raia wa kawaida wa Misri.
Licha ya udadisi uliojitokeza, mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Misri amethibitisha kuwa benki hiyo inashiriki katika mradi huwo katika ngazi ya kutoa ushauri. Alisema pia mradi wa mfereji wa Seuz utabadilisha hali ya kiuchumi nchini humo, na kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana wa Kimisri.
Mfereji wa awali uliokuwa na urefu wa maili 101 na ambao unaunganisha bara la Ulaya na Asia, ulichukua miaka 10 kujengwa wakati wa miaka ya 1860 kwa gharama kubwa ya fedha na watendaji kazi.
mwandishi: Yusra Buwayhid/ips
Mhariri:Josephat Charo